Saturday, March 22, 2014

Ndege ya Malaysia ; Msako wa wiki mbili haujaleta matunda

Ndege ya shirika la ndege la Malaysia

Wiki mbili baada ya ndege ya shirika la ndege la Malaysia kupotea ikiwa na abiria 239, maafisa wanajitarayisha na kazi ya muda mrefu,wakati msako ukiendelea na hakuna kilichopatikana zaidi ya fadhaa na maswali mapya.
Malaysia Airlines Boeing 777

Kikosi cha kimataifa kinachosaka ndege hiyo yenye namba ya safari MH370 katika eneo la ndani la bahari kusini mwa India kimerejea leo Jumamosi(22.03.2014) katika eneo ambako mabaki ambayo yanashukiwa kuwa ya ndege hiyo yalionekana kwa kupitia picha za satalaiti mapema wiki hii.
Ndege sita na meli mbili za kibiashara zinapekua eneo hilo licha ya kwamba maafisa nchini Australia wameonya kuwa vipande hivyo vilivyoonekana , kimoja kikiwa na urefu wa mita 24, huenda visihusike na ndege hiyo iliyopotea ama huenda vimezama.
Satellit Orbiting Carbon Observatory-2 OCO

Vifaa vya satalaiti angani
China, Japan na India zinatuma ndege na meli za kijeshi, Australia na China zinaelekea katika eneo hilo, zaidi ya kilomita 200 kusini magharibi mwa mji wa Perth.
Hali ya hewa
"Hali ya hewa katika eneo la msako ni nzuri, ambapo mtu anaweza kuona kwa umbali wa kilomita 10", amesema afisa wa mamlaka ya usalama wa safari za anga wa Australia Sam Cardiwell.
Ndege na meli pia zimeanza tena msako huo katika bahari ya Andaman kati ya India na Thailand, wakiingia katika maeneo ambayo tayari yamekwisha chunguzwa kuona iwapo kuwa kitu ambacho kinaweza kutengua kitendawili hicho kikubwa katika zama hizi za kisasa za usafiri wa anga.
Malaysia Suche Australien Flugzeug 20.03.2014

Ndege zikiwa kazini kusaka ndege ya Malaysia
Uwezo wa Malaysia una ukomo
Maafisa wa Malaysia wamekuwa wa kweli kuhusu uwezo wao wa kuongoza operesheni hiyo yenye uzito wa kimataifa ambapo baadhi wamesema inapindukia uwezo wa kiufundi wa nchi hiyo na utaalamu.
"Hii inaendelea kuwa juhudi ya kimataifa ikiratibiwa na Malasyia, ikihusisha nchi kadhaa kutoka duniani kote", amesema waziri wa ulinzi wa Malaysia Hishammuddin Hussein katika wakati wa kutoa maelezo kwa vyombo vya habari jana Ijumaa(21.03.2014).
Designierter US Verteidigungsminister Chuck Hagel

Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel
Malaysia imekaribisha "kila aina ya msaada kuendelea kufuatilia kila kitakachoweza kuonesha dalili ya kupata uwezekano unaoaminika kuhusu ndege hiyo", amesema Hishammuddin, ambaye pia ni waziri wa uchukuzi.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel ameihakikishia Malaysia kuwa atatafakari kutoa vifaa vya uchunguzi chini ya maji kuimarisha juhudi za kufahamu ndege hiyo ya Malaysia iko wapi.

Malaysia Suche Australien Satellitenaufnahme 20.03.2014

Kipande kinachofikiriwa kuwa ni kutoka ndege ya Malaysia iliyopotea
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Admirali John Kirby amethibitisha kuwa Hishammuddin alizungumza na Hagel juu ya msako huo wa ndege hiyo iliyokuwa ikielekea mjini Beijing ikiwa na abiria 239 ambayo ilipotea muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur Machi 8 mwaka huu.
Mwandishi Sekione Kitojo / dpae / rtre

Mhariri: Caro Robi
Chanzo: DW Swahili

No comments: