Jamaa za abiria wa ndege hiyo wamekumbwa na majonzi makubwa.
Mamlaka ya usalama wa safari za
baharini nchini Australia imesema kuwa operesheni ya kuitafuta ndege ya shirika
la Malaysia iliyotoweka imesitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa na mawimbi
makali baharini.
Taarifa zinasema kuwa upepo mkali
pamoja na mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo ina maana kuwa ndege
hazitoweza kupaa kwa usalama. Mawimbi makali yameilazimisha meli ya jeshi la
wanamaji wa Australia kuondoka katika eneo ambalo mabaki yanayodhaniwa kuwa ya
ndege hiyo yalionekana hapo jana Jumatatu.
Dr Erik van Sebille, ambaye ni
mtaalam wa maswala ya Baharini katika chuo kikuu cha New South Wales mjini
Sydney, amefanya utafiti katika eneo hilo la kusini mwa Bahari Hindi kutambua
ni wapi na vipi vifusi vinasafirishwa na mawimbi ya bahari. Anasema itakuwa
vigumu sana kupata mabaki ya ndege hiyo.
Shughuli ya kuitafuta MH370
imesitishwa
" Ni eneo lisiloweza kukalika
duniani, acha niseme. Upepo unaovuma ni mkali sana, mawimbi ni makubwa, ni
mojawepo wa mawimbi makubwa zaidi baharini. Unapofika katika eneo hili la
kusini, unaanza kuhisi athari za eneo la Antactica kwenye bahari. Hapa
tunazungumzia dhoruba kali kali sana hususan wakati huu tunapoingia majira ya
kupukutika," anasema Dr. Erik van Sebille.
Kadhalika amesema kuwa vifusi
vilivyoenekana hapo jana tayari vimekwishaondolewa katika eneo hilo na mawimbi
makali.
"Haitakuwa rahisi kabisa kupata
kijisanduku cha kunasa habari. Mawimbi ya eneo hili ni makali na kwa hiyo
vifusi ambavyo wametambua kwa sasa huenda vimehamishwa katika kipindi cha
majuma mawili au matatu tangu ndege hiyo ianguka-na huenda vimesafiri kilomita
alfu moja tayari. Na hii inaifanya vigumu kurejelea utafutaji kwa sababu bahari
inabadilika sana hapa-ina vurugu ukipenda."
Hapo awali naibu waziri wa mashauri
ya nchi za Kigeni wa China Xie Hangsheng, aliitaka serikali ya Malaysia kutoka
ushahidi unaoelezea kuwa ndege hiyo ilianguka katika eneo la Kusini mwa bahari
Hindi. Ndege hiyo ilitoweka kwenye mtambo wa Radar zaidi ya majuma mawili yaliyopita.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment