Waziri mkuu wa Uturuki Recep Erdogan,
anayekabiliwa na maandamano na kashfa za rushwa, anakabiliwa na mtihani muhimu
Jumapili(30.03.2014) wakati wapigakura milioni 50 watapiga kura katika uchaguzi
wa serikali za mitaa. Akitukuzwa kuwa ni "Sultan"
na waungaji mkono wake nchini humo na akionekana kama "dikteta" na
mahasimu wake wakubwa, Erdogan amefanya kampeni kwa wiki kadha pamoja na
wagombea wa kiti cha meya, na kuufanya uchaguzi huo kuwa ni kura ya maoni
kuhusu utawala wake wa miaka 11.
Matokeo, hususan katika mji mkubwa wa
Istanbul na Ankara, yataathiri hali yake ya baadaye wakati akilenga kugombea
kiti cha urais mwezi August, ama abadilishe sheria za chama na kugombea kipindi
cha nne akiwa kama waziri mkuu mwaka ujao.
Waziri mkuu Erdogan katika mkutano wa
kampeni
Akabiliwa na mzozo wa ndani
Miezi 10 iliyopita imekuwa ya mzozo
mkubwa kwa Erdogan, kiongozi ambaye amesifiwa nyumbani na nje ya nchi hiyo kwa
kuuendesha ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo na kubadilisha hiyo ambayo iko katika bara
la Ulaya na Asia kuwa mhusika mkubwa katika uchumi wa dunia.
Lakini tabaka la watu wa kipato cha
kati wanaoishi mijini ambao hawahusishi dini kuwa ni msingi wa maadili
limetengwa tangu polisi ilipokandamiza kwa nguvu wapinzani katika bustani ya
Gezi mjini Istanbul, na kuzusha wiki kadha za mapambano ya mitaani ambayo
yamesababisha watu wanane kupoteza maisha na wengine kwa maelfu wakiwa
wamejeruhiwa.
Maandamano mjini Ankara
Ukandamizaji huo wa nguvu ulizusha
hali inayoongezeka ya kiongozi wa kimabavu ambaye anataka kuwa mtawala pekee,
wakati akipoteza washirika wake wa zamani, hususan kiongozi wa kidini ambaye
anaishi hivi sasa katika jimbo la Pennyslvania nchini Marekani Fethullah Hulen,
ambaye ni hasimu yake mkubwa.
Chama cha AKP katika uchaguzi nchini
Uturuki
Wasaliti wa ndani
Erdogan amemshutumu imam huyo mwenye
umri wa miaka 73, pamoja na wafuasi wake katika jeshi la polisi na mahakama
nchini Uturuki , kwa kuhusika na wimbi la udukuzi na uvujaji katika mitandao ya
kijamii na kufichua rushwa na mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu usalama wa nchi
ambapo viongozi walikuwa wakizungumzia kuanzisha hatua za kijeshi dhidi ya
Syria.
Jibu la serikali , hususan kuzuwia
mtandao wa kijamii wa Twitter na YouTube katika wiki zilizopita, umezusha
shutuma kali kutoka washirika wa Uturuki wa umoja wa NATO pamoja na makundi ya
haki za binadamu. "Tutatowa somo kubwa kwa
Pennyslvania, kwa wale ambao wanadukua mawasiliano ya simu," ameapa
Erdogan katika mkesha wa uchaguzi. "Ni wasaliti ... ni
majasusi..tutashinda tena, Mungu akijalia!"
Wakati uchaguzi ukikaribia , Erdogan
mara kwa mara alisema kuwa "yeyote atakayeshinda katika mji wa Istanbul
atashinda Uturuki". Kutokana na kulakiwa kwa hamasa kubwa meya wa zamani
siku ya Jumamosi, wakati wafuasi wake wakimshangiria kwa sauti kubwa, wengine
wakipanda juu ya miti kuweza kupata kumuona , chama chake cha Justice and
Development AKP kinaonekana kuwa na nafasi nzuri ya kuendeza nafasi yake ya
ushindi katika uchaguzi.
Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe
Mhariri: Sudi Mnette
DW Swahili
No comments:
Post a Comment