Mke wa rais wa Marekani Michelle
Obama akitoa hotuba katika chuo kikuu cha Peking mjini Beijing, Machi 22, 2014
Mke wa rais wa Marekani Michelle
Obama, amewaambia wanafunzi katika taasisi ya Stanford mjini Beijing ya chuo
cha kikuu cha kifahari cha Peking kuwa uwezo wa kupata habari kupitia mtandao,
na uhuru wa kusema ni haki za wote duniani.
Katika siku ya pili ya ziara yake
huko China, Mke wa rais Obama aliwaambia wanafunzi wa Marekani na wengine leo
Jumamosi kuwa uhuru wa kujieleza na wa kuabudu, na uwezo wa kupata habari ni
haki za kimsingi cha kila mtu duniani.
Utawala wa chama cha Kikomunisti cha
China ni mojawapo ya tawala zinazodhibiti uhuru wa kusema na kupata habari,
huku ukiweka uhdibiti mkali wa habari kutoka mtandao wa internet.
Maafisa wa White House wanasema ziara
ya Michelle itatilia mkazo zaidi elimu na kuepuka maswala mengine mazito kati
ya Marekani na China kama yale ya haki za binadamu na biashara.
No comments:
Post a Comment