Viongozi wa nchi na wakuu wa serikali
kutoka duniani kote, pamoja na wajumbe wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine
kadhaa wanakutana mjini The Hague ili kujadili njia za kuzuia hatari ya
kinyuklia duniani.
Viongozi kutoka nchi 53 wanaanza
mkutano wao wa kilele katika mji wa Uholanzi wa The Hague kujadili njia za
kuzuia hatari ya silaha za nyuklia kutumiwa na magaidi.
Kwenye mkutano wao siku mbili viongozi
hao pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa pia watazungumzia juu ya
njia za kupunguza nyenzo za kinyuklia duniani ambazo siyo za kijeshi.
Marais wa Marekani Barack Obama na wa
China XI Jingping pia wanahudhuria mkutano huo.
Waziri wa mambo ya nje Urusi, Sergei
Lavrov ameshawasili mjini The Hague kwa ajili ya mkutano huo.
Rais wa China Xi Jinping, na
mwanamfalme wa uholanzi Willem Alexander
Marais hao na viongozi wengine kutoka
kote duniani kwenye mkutano wao wa siku mbili wataziangalia njia za kuhakikisha
kwamba nyenzo za kinyuklia hazingii katika mikono ya makundi ya kigaidi kama
Al-Qaeda.
Mkutano huo wa kilele unaofanyika
kila baada ya miaka mwili unafanyika kwa mara ya tatu tokea uanzishwe kutokana
na wazo la Rais Obama mnamo mwaka wa 2009.
Juhudi za kimataifa zinasonga mbele
ingawa mpaka sasa magaidi hawajafanya mashambulio kwa kutumia silaha za
nyuklia. Wataalamu wanaamini kwamba hatari ya silaha za nyuklia kutumiwa na
magaidi siyo jambo la kubuni.
Msingi wa Usalama wa nyuklia
kujadiliwa katika mkutano
Magaidi wa Chechen pia walijaribu
kuzitumia silaha za sumu mjini Moscow. Hata hivyo pana wasi wasi huenda mkutano
huo juu ya usalama wa kinyuklia ukagubikwa na mgogoro wa Ukraine. Lakini Waziri
Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte amesema mgogoro wa Ukraine hautagongana na ajenda
ya mkutano huo.
Pia ameeleza kwamba mkutano kama huo
juu ya masuala ya usalama unaweza kuwa fursa nzuri ya kuyajadili masuala
mengine vile vile kama mgogoro wa Ukraine.
Wataalamu wa silaha za nyuklia
Waziri mkuu wa Uholanzi ameeleza kuwa
viongozi wa dunia kwenye mkutano wao wa siku mbili wanatarajiwa kuweka msingi
wa usalama wa nyuklia, yaani mpango thabiti wa kuhakikisha kwamba nyenzo za
kinyuklia haziingii katika mikono ya magaidi.
Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni
zipo tani 1390 za madini ya uran duniani, yaliyorutubishwa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo pia zipo
tani 490 za madini ya Plutonium duniani. Na kati ya hizo kiasi ya tani 260
zinatumika kwa madhumuni ya amani, kama vile kwa ajili ya tiba.
Mwandishi: Over,Veronica.
Tafsiri:Mtullya Abdu.
Mhariri:Gakuba, Daniel
Chanzo: DW Swahili
No comments:
Post a Comment