Wladimir
Putin und Barack Obama am Telefon
Rais Vladimir Putin wa Urusi amefanya
mazungumzo ya simu na mwenzake wa Marekani Barack Obama na kulijadili pendekezo
la Marekani la kumaliza mgogoro wa Ukraine kwa njia ya kidiplomasia.
Ikulu ya Marekani imesema Rais Putin
amempigia simu Obama baada pendekezo lililowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje
wa Marekani kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov mapema wiki hii.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jay Carney alisema "Rais Obama amependekeza
kwamba Urusi iweke majibu madhubuti ya kimaandishi"
Viongozi hao wote wawili
wamekubaliana kwamba Waziri Kerry na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov wakutane
tena kujadili hatua nyingine kwa ajili ya kuzingatia pendekezo hilo la
kidiplomasia kwa lengo la kumaliza kabisa mgogoro wa Crimea.
Wanajeshi wa Urusi katika mgogoro
Crimea
Hata hivyo hakukuwa na zaidi kuhusu
jitihada hizo za kidiplomasia lakini taarifa ya Ikulu ya Marekani inasema Obama
ameelezea dhamira yake ya kutafuta suluhu ya kidiplomasia. Aidha inaongeza
kueleza kwamba "jambo hilo linawezekana tu pale ambapo Urusi itaondoa
majeshi yake na kutochukua hatua nyingine yoyote ya kuingia katika mipaka ya
Ukraine" imeeleza taarifa hiyo.
Baadae afisa tawala mwandamizi
alidokeza kuwa mjadala wa awali wa kuangalia uwezekano wa kutafuta suluhisho
uligusia masuala ya kupelekwa waangalizi wa kimataifa, kuondoshwa kwa majeshi
ya Urusi na kufanyika kwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Urusi na Ukraine.
Dhana ya kurudisha mataifa ya kisovieti
Kitendo cha Urusi kulichukua eneo la
Crimea kunatengeneza upya mipaka ya Ulaya na kufungua upya Vita Baridi kati ya
Mashariki na Magharibi. Msuguano wa kidiplomasia umeulazimisha Umoja wa
Kujihami NATO kutupia jicho kijeshi katika maeneo ya iliyokuwa mataifa ya
Jumuiya ya zamani ya Kisovieti kwa lengo la kudhibiti hamasa ya taifa hilo ya
kutaka kupanua mipaka yake.
Rais Putin kwa mara ya kwanza amekiri
kuwa jeshi lake lilihusika moja kwa moja katika eneo la Crimea , hatua ya awali
ambayo viongozi wenye mtazamo wa kimagharibi mjini Kiev, wanaohofia pengine ni
mpango wa kumega sehemu kubwa zaidi ya Ukraine.
Urusi kutoendeleza harakati za kijeshi
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Ban Ki-moon amesema Putin amemuhakikishia kwamba hana mpango wa
kuendelea na operesheni zake za kijeshi katika kanda hiyo. Rais Obama
alimwambia mtangazaji wa kituo cha televisheni cha CBS kwamba kuna ushahidi wa
wazi majeshi ya Urusi yanajiimarisha katika mipaka ya Ukraine.
Mapema wiki hii afisa usalama wa juu
kabisa nchini Ukraine alisema kumeonekana takribani wanajeshi 100,000 wa Urusi
katika maeneo ya karibu na Ukraine, idadi ambayo haijathibitishwa wala
kukanushwa na upande wa Urusi.
Mwandishi: Sudi Mnette AFP
Mhariri: Sekione Kitojo
DW.DE
No comments:
Post a Comment