Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Mhe. Jaji St. Damian Lubuva akiongea na vyombo vya Habari leo Mkoani
Iringa akifafanua juu ya Daftari la Kudumu la Wapiga kura Jimbo la
Kalenga.(Picha na Martha Magessa)
Baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi
kukutana na Viongozi wa Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi wa Ubunge wa Jimbo la
Kalenga mnamo tarehe 12 mach 2014, na kutoa taarifa kuhusu maadalizi ya
Uchaguzi katika jimbo hilo.
Vyama vya Siasa katika mkutano huo
viliarifu kama ilivyokuwa katika chaguzi ndugo zilizopita, daftari la kudumu la
wapiga kura litakalo tumika katika uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kalenga ni lile
lililotumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Kutokana na hoja hiyo Tume ya Taifa
ya Uchaguzi imetoa ufafanuzi kuhusu daftari la kudumu la wapiga kura
litakalotumika katika uchaguzi wa Ubunge Jimbo la Kalenga utakaofanyika 16 mach
2014.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Mhe. Jaji St. Damian Lubuva amesema kuwa, Tume kwa mamlaka iliyopew na
Sheria na Kanuni za Uchaguzi imekuwa ikipitia na kuhakiki Daftari la kudumu la
Wapiga kura lililotumika katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa dhumuni la kuondoa
kasoro ndogo ndogo zilizokuwepo katka daftari hilo.
Jaji St.Lubuva amesema, Kasoro hizo
ni kuwaondoa wapiga kura ambao taarifa zao zinatokea kwenye daftari zaidi ya
mara moja pamoja na kuweka majina ya kupiga kura ambao walijiandikisha hapo
awali na wana kadi za kupiga kura ambapo kwasababu mbalimbali za kimfumo,
majina yao hayakutokea kwenye daftari lililotumika katika Uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2010.
Ameongeza kuwa, kilichofanyika ni
uhakiki wa daftari hilo ili kuwa sahihi zaidi na kuhakikisha kila
aliyeandikishwa awali na kupewa kadi ya kupiga kura anatumia haki yake ya
kupiga kura, ili kuondokana na malalamiko ya kushindwa kupiga kura kwa sababau
ya kukosekana jina la mpiga kura katika kaftari hilo.
Aidha amesema, idadi ya wapiga kura
ni 71,957 pamoja na vituo vya kupiga kura 216 vilivyopo katika jimbo la
Kalenga.
Jaji St.Lubuva ametoaonyo rai wa
vyama vya siasa kufuata taratibu na sheria walizowekewa ili kuchaguzi ufanyike
kwa hali ya utulivu na haki pasipo uvunjifu wa amani.
Hata hivyo, amesema uchaguzi mgogo wa
ubunge utafanyika tarehe 16 machi 2014 katika Jimbo la kalenga na kuagiza vyama
vya siasa kutii agizo la kukoma kwa kampeni zao ifikapo tarehe 15 machi 2014
majira ya saa 12 jioni.
No comments:
Post a Comment