Monday, March 24, 2014

Wito watolewa kutoa maonyo zaidi kwa Russia


Maonyo kutoka maeneo mbli mbali ikiwa ni pamoja na viongozi wa muda wa Ukraine, kamanda wa juu wa kijeshi wa  NATO, na mwenyekiti wa kamati ya mambo ya usalama ya Marekani , kwamba majeshi ya Russia yanajiandaa kwenda zaidi ya Crimea yanapelekea wito wa majibu makali kutoka Washington na nchi nyingine za magharibi.

Wajumbe wa pande mbili wa bunge la Marekani wanaotembelea Kyiv wanasema wameambiwa na watu wa Ukraine waliokutana nao Jumapili  kwamba hawako tayari kuachia sehemu nyingine yeyote ya nchi hiyo na wako tayari kupambana.

Wabunge hao wawili na mwakilishi mmoja waliwaambia waandishi wa habari Jumapili usiku wana imani kwamba vikwazo vizito zaidi, na sera nyingine za kutoa adhabu chini ya utegemezi wa wenzao na muungano wa pamoja na nchi za magharibi unaweza kuwazuia Russia kufanya uchokozi zaidi.

Ngome zote kubwa za kijeshi katika Peninsula ya Crimea zilizochukuliwa na Russia wiki iliyopita hivi sasa ziko chini ya udhibiti wa majeshi ya Moscow.

Majeshi mengine ya Russia yanafanya mazoezi ya kijeshi kwenye upande wa mashariki wa Russia. Na waziri mkuu wa kujitangaza wa Crimea ametoa wito kwa raia wa Russia kutoka nchi za zamani za Urusi ya zamani, ambayo Moscow inaitangaza kama si halali.

Seneta Kelly Ayotte wa New Hampshire Mrepublikan na mwanachama wa kamati ya bunge ya usalama , amesema Marekani tayari imeonyesha nguvu zake na kuonyesha hilo na NATO itafanya zaidi kama kutakuwa na uvamizi kwa Ukraine kwenye nchi kavu.

Lakini kama kuna vita kati ya Russia na Ukraine anasema seneta Joe Donnelly mdemokrat kutoka jimbo la Indiana , wajibu utaangukia moja kwa moja kwenye mabega ya rais Vladmnir Putin wa Moscow.

Mvutano kati ya nchi hizo jirani na historia ndefu ya makubaliano ya pamoja na urithi wa Russia  inagawanya marafiki na familia.

Maafisa wa kijeshi wa Russia walikaririwa na vyombo vya habari vya serikali wakisema kwamba Moscow inakubaliana na makubaliano ya kimataifa kupunguza idadi ya majeshi yake karibu na mpaka wa Ukraine.

Lakini waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani  Frank Walter Steinmeier amesema baada ya kutembelea Ukraine kwamba ana wasi wasi Russia watakuwa wamefungua mtiririko wa muziki kujaribu kuandika upya mipaka ya kimataifa huko Ulaya.

Chanzo: VOA

No comments: