Mkuu wa Mafia Italia Salvatore Riina
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani
Papa Francis amewaonya wanachama wa genge la Mafia kwamba watakwenda motoni
iwapo hawatatubu dhambi zao.
Akizungumza katika sherehe ya maombi
ya ndugu na jamaa za waathiriwa wa genge hilo waliouawa nchini Italia,Papa
Francis amesema kuwa wanachama wa kundi hilo hawawezi kutumia fedha wanazopata
kwenda peponi.
Wakati wa ibada hiyo majina ya watu
800 waliouawa na wanachama wa genge hilo yalisomwa.
Waandishi wanasema kuwa lengo la
ibada hiyo ilikuwa kuonyesha kwamba kanisa katoliki linapinga uhalifu mbali na
kujitenga na wakuu wa genge hilo wanaodai kuwa wafuasi wakubwa wa kanisa hilo.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment