Mtoto Cyprian Osinya na kakake walikuwa kanisani wakati wa shambulizi la Jumapili
Huku hali ya taharuki ikiendelea
kutanda mjini Mombasa pwani ya Kenya ambapo magaidi walivamia kanisa siku ya
Jumapili na kuwapiga risasi waumini, mmoja wa waathiriwa wa shambulizi hilo
amefikishwa Nairobi mwa matibabu maalum.
Shirika la madaktari la AMREF,
limemleta Nairobi Mtoto Cyprian Osinya aliye na miezi kumi kutoka Mombasa kwa
matibabu maalum ya upasuaji wa kichwa baada ya madaktari kugundua kuwa risasi
imekwama katika ubongo wake.
Madkatari wanasema kuwa ubongo wa
mtoto huyo umefura na kwamba risasi iko upande wa kulia wa ubongo wenyewe.
Upasuaji unatarajiwa kufanywa baada ya wiki mbili.
Mamake aliyekuwa anamkinga kutoka kwa
magaidi waliovamia kanisa hilo siku ya Jumapili ,alifariki kanisani humo baada
ya kupigwa risasi.
Inaarifiwa risasi aliyomuingia
kichwani Cyprian ni risasi iliyomuua mamake kupitia kwa kifua chake na kuishia
katika ubongo wa mtoto huyo.
Mamake Cyprian, alikuwa miongoni mwa
watu sita waliouawa katika shambulizi hilo, baada ya washukiwa watatu wa ugaidi
kulivamia kanisa la Joy in Jesus katika mtaa wa Likoni na kuanza kuwafyatulia
waumini risasi kiholela.
Cyprian atafanyiwa upasuaji maalum
katika hospitali kuu ya Kenyatta mjini Nairobi ambao utagharamiwa na serikali.
No comments:
Post a Comment