Wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya
Misri imesema kuwa inachunguza maneno yanayoandikwa kwenye mitandao ya kijamii
yakiwa na kitambulisho, yaani "hashtag", yanayomtusi waziri wa ulinzi
aliyestaafu ili kugombea urais, Field Marshall Abd-el-Fattah el-Sisi.
Heshtegi hiyo ambayo tafsiri yake ni
"mpigie kura kuwadi", imesambazwa kwenye Twitter zaidi ya mara
100-milioni na imependwa na watu zaidi ya 40,000 kwenye Facebook.
Inaarifiwa kuwa wizara ya mambo ya
ndani ya Misri imesema itawakamata watu wanaoitumia sana heshtegi hiyo.
Maneno hayo piya yamekuwa yakichorwa
kwenye kuta za mjini Cairo chini ya mabiramu ya picha za Bwana Sisi.
Field Marshall E-Sisi aliipindua
serikali iliyochaguliwa kwa njia za kidemokrasi ya Mohamed Morsi wa Muslim
Brotherhood mwezi Julai mwaka jana.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment