Kundi la G-7
Viongozi wa kundi la mataifa saba
tajiri zaidi duniani, G-7, wanafanya mazungumzo kwa siku ya pili mfululizo hivi
leo mjini Hague, Uholanzi ajenda kuu ikiwa ni hatua ya Urusi kunyakua jimbo la
Crimea kutoka Urusi.
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998,
Moscow imenyimwa kiti katika kongamano hilo. Mkutano wa dharura wa G-7
uikubaliana kufutilia mbali kundi la G-8, kundi la mataifa manane tajiri zaidi
duniani, ambalo linaishirikisha Urusi.
Viongozi wa mataifa ya kundi hilo
wameonya kuwa vikwazo zaidi vitatolewa iwapo Urusi itaingia maeneo ya mashariki
au Kusini mwa Ukraine ikiwepo kulenga sekta ya kawi nchini Urusi. Lakini
Marekani kadhalika imesisitiza kuwa fursa ya kusuluhisha mzozo huo wa njia ya
kidiplomasia ingalipo.
No comments:
Post a Comment