HABARI KAMILI
Bunge la Kenya lenye wabunge wengi
wanaume limeidhinisha mageuzi yenye utata katika mswada wa ndoa ambayo yatawapa
wanaume usemi zaidi katika familia na uhusiano mwingine katika jamii.
Wabunge wanaume waliungana kupitisha
mageuzi hayo ambayo yataathiri pakubwa familia kwa ujumla
Wabunge wanaume walipitisha mswada
mpya wa ndoa baada ya kuufanyia mageuzi na kuruhusu wanaume kuoa zaidi ya
mwanamke mmoja bila ya kushauriana na mke wa kwanza. .
Wabunge wanawake waliondoka katika
kikao hicho kwa hasira wakiahidi kuubadili mswada huo.
Pia sehemu za sheria ya ndoa ambazo
zinasema kuwa wanandoa waweze kugawana mali yao wanapoachana imelegezwa.
Wanawake wameahidi kubadili kufutilia
mbali mswada huo
Mswada wenyewe awali uliruhusu
wanaume kuoa wanawake zaidi ya mmoja lakini ukasisitiza kuwa mke wa kwanza
sharti ashaurie kabla ya mumewe kuoa mke wa pili au wa tatu.
Mmoja wa wabunge wanawake alisema
kuwa ni muhimu mageuzi hayo katika mswada huo kutupiliwa mbali kwa ajili ya
kulinda familia.
''Ni muhimu kumuomba mkeo wa kwanza
ruhusa kabla ya kuoa mke wa pili,'' alisema mbunge huyo. Lakini mbunge mmoja
mwanamume, Benjamin Washiali, alisisitiza kuwa yeye ni mtoto wa mke wa pili
katika familia yao. ''Ikiwa sheria hii ingekuwepo mimi nisingezaliwa.''
Wabunge wengi wanaume wamesema kuwa
ni jambo la kawaida kwa wanaume wa kiafrika kuwa na wake zaidi ya mmoja.
Wanawake bungeni sasa wanasema
watajitahidi kuhakikisha kuwa mswada huo unatupiliwa mbali.
Nini maoni yako kuhusu hoja hii? Tupe
maoni yako kwenye mtandao wetu wa Facebook Bofya
https://www.facebook.com/pages/BBC-Swahili/160894643929209?ref=hl
No comments:
Post a Comment