Meli ya kivita ya Ukraine
Bendera za Urusi kwa hivi sasa
zinapeperushwa katika vituo vya kijeshi mjini Crimea, wakati ambapo Urusi
ikiilalamikia Ukraine kwa kukiuka mikataba ya kimataifa ya usafiri wa anga na
kuyaweka hatarini maisha ya marubani
Tangazo la kupeperushwa kwa bendera
za katika vituo vya kijeshi katika mjini Crimea la afisa wa juu kabisa wa jeshi
Jenerali Valery Gerasimov lilisema mpaka sasa wanadhibiti maeneo yote ya
kijeshi katika eneo hilo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo bendera ya Urusi kwa hivi
sasa inapepea katika katika vituo vyote 193 vya kijeshi mjini Crimea. Taarifa
ya mkuu huyo iliongeza kusema bendera zilipandishwa katika hafla iliyoambatana
na uimbaji wa wimbo wa taifa.
Shirika la habari la RIA novosti
limemnukuu kamanda Gerasimov akiesema wale wanajeshi wa Ukraine wanaotaka
kuondoka katika eneo hilo wako huru kufanya hivyo kwa kutumia usafiri wa reli
na watajizaja nafasi hizo mara moja pale itakapobainika hawapo kazini.
Ameongeza kusema kiasi ya wanajeshi 1,500 wa Ukraine ambao wamekuwa wakifanya
kazi katika serikali ya Ukraine, katika kituo kilichopo mjini Simferopol kwa
ajili ya kuandaa safari yao.
Maandalizi ya jeshi la Ukraine
Ukraine Interim Präsident Alexander
Turtschinow 23.02.2014 2013
Rais wa Mpito wa Ukraine Alexander
Turtschinow
Naye kaimu rais wa Ukraine, Oleksandr
Turchynov ameliomba bunge la taifa lake kupitisha idadi fulani ya wanajeshi
ambao watashirikia mazoezi ya pamoja na jeshi la Umoja wa kujihami wa NATO, kwa
lengo la kuweka uwiano ulio sawa na jeshi la Urusi katika eneo la Crimea.
Ombi hilo la Turchynov linaelezwa
kutokana na tangazo hilo la Urusi la kudhibiti vituo vyote vya kijeshi katika
eneo la Crime. Kiongozi hiyo amesema Ukrine itafanya awamu mbili za mazoezi ya
kijeshi na Marekani katika kipindi cha msimu wa kiangazi.
Serikali ya Marekani mwezi huu
ilipendekeza kutumia asilimia 28 katika bajeti yake ya wizara ya ulinzi katika
jitihada za kubadili mfumo wa kijeshi kuwa wa kisasa nchini Ukraine na katika
mataifa mengine yalikuwa katika muungano wa kisovieti wa zamani.
Katika hatua nyingine, Wizara ya
Mambo ya Nje ya Urusi imesema maafisa wa uhamiaji nchini Ukraine wamewazuia
wahudumu wa ndege ya abria ya Urusi kutoka katika ndege hiyo baada ya ndege
hiyo kutua mjini Kiev. Taarifa hiyo imesema kitendo hicho ambacho hakukutolea
taarifa za kina kina hatarisha usalama wa abiria. Kwa mujibu wa kanuni za
usafiri marubani na wahudumu wa ndege za abiria wanapaswa kupumzika kabla ya
kuanza safari nyingine.
Mapema wiki hii, wizara hiyo ilitoa
taarifa iliyosema kwamba raia wa Urusi wamekuwa wakiwindwa nchini Ukraine na
kuulalamikia utawala wa Ukrain kwa kutokuwa na uwezo au nia ya kutaka kuvizuia
vitendo hivyo. Urusi imekuwa ikitumia ripoti inayosema watu wenye asili ya
Kirusi nchini Ukraine wapo katika kitisho jambo ambalo limeonekana kama sababu
ya kulitwaa eneo la Crimea.
Mwandishi: Sudi Mnette AFP/RTR
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
DW.DE
No comments:
Post a Comment