Maafisa wa idara ya ulinzi kwa Obama
wakimuandalia njia yakupita
Maafisa watatu kutoka katika idara ya
kumlinda Rais wa Marekani Barack Obama katika ziara yake nchini Uholanzi,
wamerejeshwa nyumbani kwa kosa la utovu wa nidhamu.
Jarida la Washington Post nchini
Marekani limeripoti kwamba mmoja wa askari hao alipatikana akiwa mlevi chakari
kiasi cha kupoteza fahamu katika hoteli moja mjini Amsterdam.
Mapema Jumapili, siku moja kabla ya
Obama kuwasili nchini humo, wafanyakazi wa hoteli waliarifu ubalozi wa Marekani
nchini Uholanzi kuhusu walivyompata askari huyo katika hali ya kutojitambua.
Msemaji wa idara ya upelelezi
Marekani alikataa kutoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo, ingawa alisisitiza
kuwa watatu hao wameachishwa kazi kwa muda uchunguzi ukiendelea.
Tukio hilo lilitokea kabla ya Rais
Obama kuwasili Uholanzi kwa mkutano kuhusu kawi ya Nuklear.
Shirika hilo la ujasusi limekuwa
likijaribu kujisafishia sifa yake hasa baada ya kukumbwa na kashfa mbali mbali.
Mnamo mwaka 2013, majasusi wawili
waliondolewa katika kikosi cha ulinzi cha Rais Obama kufuatia tuhuma za
kuhusika na kashfa ya ngono na utovu wa nidhamu.
Na mnamo mwaka 2012, majasusi kadhaa
waliachishwa kazi kufuatia madai kuwa walikodi makahaba walipokuwa mjini
Cartagena, Colombia.
No comments:
Post a Comment