Askari wa Ukrainer karibu na mpaka wa Russia March 21, 2014.
Maonyo kutoka maeneo mbli mbali ikiwa
ni pamoja na viongozi wa muda wa Ukraine, kamanda wa juu wa kijeshi wa NATO, na mwenyekiti wa kamati ya mambo ya
usalama ya Marekani , kwamba majeshi ya Russia yanajiandaa kwenda zaidi ya
Crimea yanapelekea wito wa majibu makali kutoka Washington na nchi nyingine za
magharibi.
Wajumbe wa pande mbili wa bunge la
Marekani wanaotembelea Kyiv wanasema wameambiwa na watu wa Ukraine waliokutana
nao Jumapili kwamba hawako tayari
kuachia sehemu nyingine yeyote ya nchi hiyo na wako tayari kupambana.
Wabunge hao wawili na mwakilishi
mmoja waliwaambia waandishi wa habari Jumapili usiku wana imani kwamba vikwazo
vizito zaidi, na sera nyingine za kutoa adhabu chini ya utegemezi wa wenzao na
muungano wa pamoja na nchi za magharibi unaweza kuwazuia Russia kufanya
uchokozi zaidi.
Ngome zote kubwa za kijeshi katika
Peninsula ya Crimea zilizochukuliwa na Russia wiki iliyopita hivi sasa ziko
chini ya udhibiti wa majeshi ya Moscow.
Majeshi mengine ya Russia yanafanya
mazoezi ya kijeshi kwenye upande wa mashariki wa Russia. Na waziri mkuu wa
kujitangaza wa Crimea ametoa wito kwa raia wa Russia kutoka nchi za zamani za
Urusi ya zamani, ambayo Moscow inaitangaza kama si halali.
Seneta Kelly Ayotte wa New Hampshire
Mrepublikan na mwanachama wa kamati ya bunge ya usalama , amesema Marekani
tayari imeonyesha nguvu zake na kuonyesha hilo na NATO itafanya zaidi kama
kutakuwa na uvamizi kwa Ukraine kwenye nchi kavu.
Lakini kama kuna vita kati ya Russia
na Ukraine anasema seneta Joe Donnelly mdemokrat kutoka jimbo la Indiana ,
wajibu utaangukia moja kwa moja kwenye mabega ya rais Vladmnir Putin wa Moscow.
Mvutano kati ya nchi hizo jirani na
historia ndefu ya makubaliano ya pamoja na urithi wa Russia inagawanya marafiki na familia.
Maafisa wa kijeshi wa Russia
walikaririwa na vyombo vya habari vya serikali wakisema kwamba Moscow
inakubaliana na makubaliano ya kimataifa kupunguza idadi ya majeshi yake karibu
na mpaka wa Ukraine.
Lakini waziri wa mambo ya nje wa
Ujerumani Frank Walter Steinmeier
amesema baada ya kutembelea Ukraine kwamba ana wasi wasi Russia watakuwa
wamefungua mtiririko wa muziki kujaribu kuandika upya mipaka ya kimataifa huko
Ulaya.
Chanzo: VOA Swahili
No comments:
Post a Comment