Mkuu wa mkoa wa Mara, Bw. John
Gabriel Tuppa.
MKUU wa mkoa wa Mara, Bw. John
Gabriel Tuppa, amefariki dunia ghafla leo majira ya saa 4.30 asubuhi baada ya
kuugua kwa muda mfupi ugonjwa wa shinikizo la damu akiwa wilaya ya Tarime
mkoani Mara.
Katibu tawala wa mkoa wa Mara, Bw.
Benedict Ole Kuyan, amesema kuwa Bw. Tuppa kabla ya kifo chake leo asubuhi
akiwa na afya njema alifika katika ofisi ya za mkoa na kumuaga kuwa anakwenda
kufunga mafunzo ya mgambo katika kijiji cha Nyamwaga wilayani Tarime.
Amesema kuwa muda mfupi baada ya
kufika katika ofisi ya mkuu wa wilaya, alipatwa na tatizo la ugonjwa huo na
muda mfupi alikimbizwa hospitali ya Tarime lakini alifariki wakati akipatiwa
matibabu.
Katibu tawala huyo amesema mwili wa
marehemu unasafarishwa kutoka Tarime kuja hospitali ya Musoma kwa ajili ya
kuhifadhiwa wakati taratibu nyingine na maelekezo ya kiserikali yakisubiriwa
kutolewa.
No comments:
Post a Comment