BAADHI ya wahitimu wa elimu juu
hawana uelewa na ufahamu wa kutosha wa kile walichokisomea na mambo
yanayoendelea kwenye mazingira husika.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Riziki Abrahamu,
alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
“Ubora wa wahitimu wanaomba kazi
kupitia chombo hiki wamekuwa hawana uwezo wa kitaalamu, ufahamu, kutotilia
maanani vigezo na masharti ya tangazo, kutojiamini, uwezo mdogo wa mawasiliano
ikiwemo matumizi ya lugha sahihi na kuamini kuwa vyeti vinaweza kuwasaidia
kupata kazi kwa urahisi,” alisema.
Alisema wahitimu wengi kutokuwa na
maandalizi sahihi na kukosa sifa halali za kitaaluma huchangia kughushi baadhi
ya sifa kwa lengo la kujipatia ajira.
“Hali hii inatisha na
inatudhirihishia kwamba wahitimu wetu wanasoma kwa kufuata mkumbo, lakini si
kuelewa kile wanachosomea,” alisema.
Chanzo: Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment