NA Ausi Chiwambo
Kwa Ufupi
Hotuba ya Rais Kikwete iliyotolewa
siku chache zilizopita imeleta mvutano miongoni mwa watanzania huku vyombo vya
habari navyo vikiwa vimegawanyika katika pande mbili yaani vinavyounga serikali
mbili na vile vinavyounga serikali tatu.
HABARI KAMILI
Nchi ya Tanzania inapita kipindi
kigumu sana hasa wakati huu Bungemaalumu la katiba likiendelea na kazi zake huku kukiwa
na mvutano wa wazi kati ya wanaopina serikali mbili na wanaopenda serikali
tatu. Mvutano huu umeanza kuwa mkubwa hasa baada ya Rais Wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya M. Kikwete kutoa hotuba yake iliyolenga haja ya
kuwa na serikali tatu.
Mara baada ya kutolewa kwa hotuba
hiyo Watanzania wamegawanywa katika makundi mawili yaani wale wanao unga serikali
mbili na wale wanaopendekeza serikali tatu. Vita hivyo vimeendelea kusikika si
tu katika ndani ya Bunge Maalumu la Katiba bali hata vyombo vya habari
vimeingia katika mvutano mkali huku baadhi ya vyombo vya habari vikirusha kwa
mtanzamo wa serikali mbili na vingine serikali mbili.
Ikumbukwe kwamba sisi sote ni
Watanzania na lengo letu ni kupata katiba mpya,hivyo vyombo vya habari kwa
tafsiri ya neon la kiingereza “The voice
of the voiceless” nikimaanisha Kipaza
sauti kwa wale wasiojiweza hasa wananchi havina budi kujenga maslahi ya
Watanzania kwanza na si kuingia katika vita baina ya vyombo hivyo vya habari
kama vile Magazeti, Radio, pamoja na Televisheni.
Kutokana na kinachoendelea inaonyesha
wazi kuwa hata taaluma yetu ya uandishi wa habari ni ya Kikanyanja maana tupo
tayari kuingia mikononi mwa wanasiasa na sio kuangalia maslahi ya Watanzania.
Waandishi tujiulize swali moja kuwa hivi taaluma yetu ni kwa ajili ya maslahi
ya Watanzania au kwa maslaya ya wanasiasa na wamiliki wa vyombo vya habari?
TUME YA KUKUSANYA MAONI YA WATANZANIA
Hoja ya kuwepo kwa katiba mpya kwa
mara ya kwanza ilisikika kutoka kwa Rais Kikwete kuwa kuna haja ya Watanzania
ijapokuwa haikuwepo katika Ilani ya Uchaguzi wa CCM (Chama Cha Mapinduzi) bali
ilikuwa kwa busara za Rais peke yake. Hii yote ilitokana na msukumo mzito
kutoka vyama pinzani vikiwemo Chama cha CUF, NCCR Mageuzi, na Chadema.
Baada ya hoja hizo Rais Kikwete
aliamua kutoa hoja ya kuwa na mchakato wa katiba mpya. Tume ya kukusanya maoni
ya Wananchi iliundwa ikiwa na lengo la kupata maoni ya Watanzania ili kupata
katiba ya Watanzania na si kama katiba ya mwaka 1977 iliyotungwa na jopo la
watu 20. Hivyo kwa busara za Rais aliona kuna umuhimu wa kupata maoni ya
Watanzania ili waseme aina ya katiba wanayoipenda.
Tume ilianza kazi zake na kuweza
kuzunguka nchi nzima na kupata rasimu ya kwanza nay a pili ikiwa na maoni ya
Watanzania wa kila hali. Tume imamaliza kazi yake na kazi iliyopo ni ya Wabunge
kati ya kusaliti maoni ya Watanzania na kuingiza yao au kuyafanyia kazi maoni
ya watanzania. Picha na kitendawili kilianza kuonekana wiki moja iliyopita mara
baada ya Jaji Joseph Warioba kutoa hotuba yake ndani ya Bunge la Katiba na
kueleza Watanzania Wamependekeza nini huku msimamo wao ni serikali Tatu.
Na ikumbukwe kwamba Tume mbalimbali
zilizoundwa hapo nyuma ikiwemo ya Jaji
Nyarali zilipendekeza kuwa Watanzania wanahitaji serikali tatau yaani ya
Tanganyika, Zanzibar, pamoja nay a Muungano. Siku ya ijumaa ya wiki iliyopita Rais Kikwete naye
alitoa hotuba yake ili kufungua bunge. Hotuba ya Rais ilipendekeza umuhimu wa
kuwa na serikali mbili ile hali tume ilipendekeza serikali tatu.
Hapo ndipo Watanzania wanaposhuhudia mvutano wa Wabunge
ndani ya Bunge la Katiba, Wanaharakati na Wasomi mbalimbali huku hata vyombo
vya habari navyo vikiwa vimegawanyika mapande mapande hasa baada ya hotuba ya
Rais kutolewa.
Ni maoni yangu kwamba Watanzania wa
leo wanatambua kila kitu kinachoendelea. Na kuja na katiba mbaya ni mwanzo wa
kuanza mchakato wa katiba mpya nyingine itayokuwa ya wananchi na sio ya chama Fulani.
Imeandikwa na
Ausi Chiwambo
No comments:
Post a Comment