Uiwindanji haramu wa Ndovu haujaathiri tu Kenya bali Afrika
nzima
Kenya inajiandaa kuanzisha mradi wa
kutumia ndege zisizokuwa na rubani kuimarisha ulinzi katika mbuga za wanyama,
kutokana na kuongezeka kwa visa vya uwindaji haramu.
Mwaka huu pekeee, zaidi ya Vifaru
kumi na wanane na Ndovu hamisini na tisa wameuawa huku pembe na meno zao
zikiibiwa na kusafirishwa kimagendo hadi nchi za ng'ambo.
Tatizo hili limekithiri sana hali
iliyomfanya Rais wa Kenya kutoa wito kwa nchi za afrika mashariki kuimarisha
uhusiano wao katika harakati za kutokomeza Ujangili.
Katika kipindi cha miezi mitatu ya
kwanza mwaka huu, Kenya imepoteza Vifaru kumi na wanane na Ndovu hamsini na
moja kwa wawindaji haramu ukilinganisha na Vifaru 59 na Ndovu 302 waliouawa
mwaka uliopita.
Viwango vya uwindaji haramu nchini
kenya na katika kanda ya kusini mwa jangwa la sahara vimeongezea katika miaka
ya hivi karibuni huku tani kadhaa za pembe za Vifaru na meno ya tembo zikinaswa
na maafisa wa ulinzi.
Naibu mkurugenzi mkuu wa shirika la
wanyama pori nchini Kenya Benjamin Kavu anasema kuwa kuzuia uwindaji haramu
imekuwa vigumu kwa kuwa hawana vifaa vya kisasa .
Na ili kukabiliana na tatizo hili, la
uwindaji haramu, shirika na wanyama pori nchini Kenya KWS pamoja na hifadhi za
kibinafsi zimeanzisha mpango wa kutumia ndege zisizokuwa na rubani, ili
kuimarisha ulinzi katika mbuga za wanyama.
Tayari majaribio ya ndege hizo
yamefanyika katika mbuga ya Ol pajeta na shirika la KWS linatarajiwa kufanya
zoezi kama hilo hivi karibu katika mbuga ya Tsavo.
Licha ya kuongezeka kwa idadi ya
Vifaru na Ndovu wanaouawa nchini Kenya shirika la KWS limesema kuwa Kenya
ingali na idadi ya kutosha kulingana na takwimu za kimataifa na kuwa
wameimarisha msako wao dhidi ya wawindaji haramu na wale wanaofadhili shughuli
hiyo.
Hata hivyo bei ya juu ya pembe za
Vifaru na meno ya tembo imechangia tatizo hili kukithiri.
Akihutubua bunge la afrika mashariki
mjini Arusha, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameelezea masikitiko yake kuhusiana
na kuongezeka la visa vya Tembo na Vifaru kuuawa.
Rais Kenyatta amesema serikali yake
itashirikiana na jamii ya kimataifa ili kusitisha biashara ya pembe za faru na
Tembo.
No comments:
Post a Comment