Waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak
Shirika la ndege la Malaysia
limewaambia jamaa na familia za abiria waliokuwa wanasafiri kwa ndege
iliyotoweka MH370 kwamba ndege hiyo imepotea na kwamba hakuna manusura.
Tangazo hilo limetolewa kwa familia
hizo kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi , ambao BBC iliweza kuuona.
Ndege ya Malaysia MH320 ilitoweka
ikiwa na abiria 239 baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur
tarehe 8 mwezi huu.
Aidha tangazo hilo limekuja huku
juhudi za kutafuta mabaki ya ndege hiyo Kusini mwa Bara Hindi zikimalizika kwa
siku ya tano bila mafaniko.
Waziri mkuu wa Malaysia amesema kuwa
ndege hiyo ilianguka Kusini mwa Bahari Hindi, bila ya manusura wowote.
Aliambia waandishi wa bahari kuwa
udadisi uliofanyiwa data ya Satelite kutoka Uingereza ndio umewathibitishia
kwamba ndege hiyo ilimalizia safari yake Magharibi mwa mji wa Perth mbali na
eneo lolote la kutua.
Ameomba vyombo vya habari kuheshimu
familia za watu waliokuwa ndani ya ndenge hiyo, akisema kuwa anasikitishwa sana
kwani kipindi chote walichosubiri taarifa njema , mwishowe imekuja kuwa taarifa
mbaya hata zaidi.
Ndege ya Malaysia MH-370, ilipoteza
mawasiliano wiki mbili zilizopita na meli za nchi mbali mbali pamoja na ndege
zimekuwa zikitafuta angalau mabaki ya ndege hiyo bila ya kupata chochote.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment