Al Shabaab
Wanajeshi wa Muungano wa Afrika
wanameuteka mji muhimu wa Koryoley, ulio umbali wa kilomita 90 Kusini Magharibi
mwa mji mkuu Mogadishu.
Mji wa Koryoley, umekuwa chini ya
udhibiti wa kundi la wanamgambo la Al Shabaab kwa miaka mitano iliyopita.
Mwandishi wa BBC aliye katika eneo
hilo anasema kulikuwa mlio wa silaha na baadhi ya raia wa mji wamekimbia.
Kutekwa kwa mji huo ni ukombozi tangu
kuanza harakati hizo dhidi ya Al Shabaab mwezi Machi mwaka jana wakiungwa mkono
na Umoja wa Mataifa.
Wanajeshi hao wamefanikiwa kukomboa
miji mingine muhimu na hata kuwatimua wapiganaji hao kutoka katika ngome zao
kubwa.
Wengi wa wanajeshi wa AU ni kutoka
Uganda, wakisaidiwa na wanajeshi wa Kenya, Burundi na sasa Ethiopia pamoja na
wanajeshi wa Somalia.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment