Popo hutumiwa kutengeza kitoweo
maarufu sana katika baadhi ya maeneo ya Guinea, lakini sasa inahofiwa kuwa popo
wanachangia kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola kusini mwa nchi hiyo.
Maafisa nchini humo sasa wamepiga
marufuku uuzaji na ulaji wa nyama ya popo katika juhudi za kudhibiti ugonjwa
hatari wa Ebola, ambao kufikia sasa umesababisha vifo vya watu 62.
Nchi za kanda hiyo zikiwemo Liberia
na Sierra Leone, zimechukua hatua kabambe kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa
huo zikiwemo kuwafanyia uchunguzi wa kiafya watu wanaongia mipakani.
Maafisa wa afya wanapata msaada
kutoka shirika la afya duniani na ujumbe wa kuhamasisha watu unapeperushwa
kupitia televisheni.
Watu watano kati ya sita walioingia
nchini Liberia kutoka Guinea walikua na ishara za ugonjwa huo na
wamethibitishwa kufa.
Hatahivyo maafisa wa utawala nchini
Liberia bado hawajathibitisha kikamilifu kama kweli walikufa kutokana na
ugonjwa wa Ebola.
No comments:
Post a Comment