Mwenyekiti wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia Front
National,Marine Le Pen
Chama cha siasa kali za mrengo wa
kulia nchini Ufaransa FN kimezusha maajabu katika chaguzi za mabaraza ya miji
zilizogeuka onyo kwa chama tawala cha kisoshialisti na kuwaruhusu wafuasi wa
kihafidhina kusonga mbele.
Chama cha Front National
kinachoongozwa na Marine Le Pen kimefaidika na ile hali kwamba idadi kubwa ya
wapiga kura hawakuteremka vituoni, wakichoshwa na kashfa kadhaa zinazokigubika
chama cha kihafidhina
Tukio jengine la kustaajabisha ni
idadi ndogo ya wapiga kura walioteremka vituoni: asili mia 38.72 ya wapiga kura
wameamua kutoteremka vituoni-
Mrengo wa shoto umepata pigo kubwa
kupita kiasi katika wakati ambapo rais Francois Hollande amepoteza vibaya sana
umashuhuri wake,miaka miwili tu baada ya kuingia madarakani .
Mijini
Perpignan,Avignon,Forbach,Béziers,Fréjus,na Tarascon chama cha siasa kali za
mrengo wa kulia FN kinaongoza matokeo ya duru ya kwanza.Na kina nafasi nzuri ya
kushinda kwengineko pia baada ya ushindi wa moja kwa moja katika mji wa
Hénin-Beaumont katika jimbo la kaskazini la Pas de Calais ambako Steeve Briois
amekipatia ushindi chama hicho kwa mara ya kwanza katika mji wenye wakaazi
zaidi ya elfu kumi.
Washoshialisti wajiweke matumaini
Paris
Wagombea wawili wa nafasi ya meya wa
jiji la Paris(kushoto) Nathalie Kosciusko-Morizet wa chama cha kihafidhina cha
UMP na (kulia) Anne HIdalgo Kombo wa chama cha kisoshialisti-.PS
Mjini Paris mgombea wa chama cha UMP
Nathalie Kosciusko-Morizet anaongoza mbele ya mgombea wa chama cha
kisoshiaalisti Anne Hidalgo.Hata hivyo mrithi wa meya aliyemaliza mhula wake
Bertrand Delanoe anapewa nafasi nzur ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi
itakapoitishwa jumapili ijayo.
"Hatukutarajia" amesifu M
arine Le Pen aliyeutaja uchaguzi huo kuwa wa aina pekee na uliomaliza enzi za
vyama viwili vya kisiasa.
Kwa mujibu wa matokeo ya muda
yaliyotangazwa usiku wa manane wa kuamkia leo na waziri wa mambo ya ndani
Manuel Valls,mrego wa kulia umejikingia asili mia 46,54,mrengo wa shoto asili
mia 37.74,siasa kali za mrego wa kulia 4.65 na siasa kali za mrengo wa shoto
asili mia0.58.
Serikali huenda ikabadilishwa
Rais wa Ufaransa Francois Hollande
Wapiga kura milioni 45 wa Ufaransa na
wale wa nchi za Umoja wa ulaya waliakiwa wakatoe sauti zao wakati wa uchaguzi
huo ambao unaangaliwa kama kipimo cha umashuhuri wa rais Francois Hollande
tangu alipochaguliwa mwezi Mai mwaka 2012.
Rais Francois Hollande huenda
akalifanyia mageuzi baraza la mawaziri."Hali inatisha" amesema
msemaji wa serikali Nadjat Vallaud Belkacem.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP
Mhariri:Yusuf Saumu
Chanzo: DW Swahili
No comments:
Post a Comment