Kundi la Anti-Balaka
Mkuu wa vikosi vya Afrika vya kulinda
amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ,amesema kuwa vijana wa kulinda amani wa
kikristo wanaojulikana kama anti-balaka,watatambulika kama maadui kutoka sasa.
Tangazo hilo la Jean -marie Michel
Mokoko linajiri baada ya kadhaa za mapigano ambayo yamesababisha mauaji ya watu
20.
Kundi la Anti-balaka limefanya
mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya waislamu baada ya waasi wa kiislamu wa
kundi la seleka kuchukua mamlaka mwaka mmoja uliopita.
Jenerali Mokoko pia amelilaumu kundi
hilo la anti-balaka kwa kutekeleza mashambulizi dhidi ya vikosi vya kulinda
amani vya Afrika vinavyoshirikiana na wenzao wa Ufaransa ili kuzipokonya silaha
pande husika.
Mkuu wa kamati ya kimataifa ya
shirika la msalaba mwekundu Peter Maurer ameanza ziara yake ya siku tatu nchini
humo. Kamati hiyo inasema kuwa taifa hilo linakumbwa na janga la kibinaadamu.
No comments:
Post a Comment