Mgomo wa walimu nchini Uingereza
Maelfu ya watoto nchini Uingereza na
Wales, wanakabiliwa na tisho la kukosa elimu huku walimu wao wakigoma.
Walimu hao wanagoma wakitaka nyongeza
ya mishahara, malipo mazuri ya uzeeni na kuboreshwa kwa mazingira ya kazi.
Wanachama wa chama cha walimu, (NUT)
watashiriki katika mgomo huo huku wakiacha shule nyingi bila walimu huku masomo
yakisitishwa.
Walimu hao wamesema hawakuwa na budi
ila kuondoka kazini kwani hakuna suluhu la matatizo yao.
Wizara ya elimu hata hivyo imelalamika
ikisema kuwa mgomo huo unaathiri maisha ya wazazi na elimu kwa watoto.
Mgomo huu ulianza baada ya walimu
kukubaliana kupiga kwa kura mwezi Mei 2011 na Juni 2012.
Asilimia 92 ya walimu walipiga kura
ya ndio kwa gomo kufanyika.
Chama cha walimu nchini humo kimekuwa
kikivutana na serikali kwa miaka miwili sasa na hata kufanya migomo
midogomidogo hadi mgomo huu mkubwa ukafikiwa.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment