Wapiganaji wa Taliban
Kundi la waakilishi wa serikali
nchini Pakistan linasafiri kuelekea katika eneo la wapiganaji wa Taliban
Kaskazini Magharibi mwa taifa hilo.
Kundi hilo linaelekea huko ili
kufanya mashauriano ya amani na kundi la wapiganaji wa kiislamu nchini
Pakistan.
Hii ni mara ya kwanza kwa waakilishi
wa serikali kufanya mkutano wa moja kwa moja na kundi la wapiganaji wa
Tehreek-i-Taliban.
Mazungumzo hayo ni harakati za waziri
mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif, kutafuta mbinu ya kukomesha ghasia ambazo
zimesababisha vifo vya watu wengi.
Wajumbe hao wa serikali waliondoka
mapema leo kuelekea katika eneo lisilojulikana Kaskazini magharibi mwa pakistan
ili kukutana na wanachama wa baraza la kisiasa la Taliban.
Ajenda ya mkutano huo hata hivyo
haijawekwa wazi,lakini inadaiwa kushirikisha makubaliano ya kuongeza mda wa
kusitisha vita ambayo yanatarajiwa kukamilika wiki ijayo mbali na kuachiliwa
kwa wafungwa wa kisiasa.
Askari jeshi katika eneo
lililoshambuliwa na Taleban nchini Pakistan
Kundi la taliban linataka watu
linaowataja kuwa 'wasiopigana' kama vile wanawake na watoto waachiliwe.
Lakini serikali imekana kumzuia
mwanamke yeyote ama mtoto katika jela zake.
Wachanaguzi wanasema kuwa serikali
nayo itataka kundi hilo kuwaachilia waathiriwa wa utekaji nyara akiwemo mwana
wa aliyekuwa waziri mkuu.
Mwezi uliopita ,baraza hilo la
wapiganaji wa taliban lilitoa matakwa yake ikiwemo kuwekwa kwa sheria ya
kiislamu nchini humo,serikali ya Pakistan kuwaondoa wanajeshi wake katika
maeneo ya vijiji mbali na serikali hiyo kuvunja uhusiano wake na Marekani.
Katika majuma matatu ambayo
makubaliano hayo ya kusitisha vita yaliafikiwa,kumekuwa na mashambulizi mabaya
katika mji wa Islamabad na Peshawar,hata hivyo kundi la Tailban limekana
kutekeleza mashambulizi hayo.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment