Athari ya maporomoko Marekani
Maafisa wa utawala katika jimbo la
Washington nchini Marekani, wamepata miili sita zaidi baada ya maporomoko ya
ardhi yaliyotokea siku ya Jumamosi.
Hii imefikisha idadi ya watu
waliofariki kutokana na maporomoko hayo hadi 14.
Watu 176 bado hawajapatikana baada ya
ukuta wa matope wenye urefu wa futi 177 kuporomoka karibu na mji wa Oso,
Kaskazini mwa Seattle.
Waokozi wangali wanaendelea na
shughuli ya kuwatafuta manusura kwa kutumia helikopta na miale ya Laser.
Lakini maafisa wanakiri kuwa wana
matumaini madogo sana ya kupata manusura.
Rais Barack Obama ametangaza hali ya
hatari katika jimbo hilo na kuwaamuru maafisa wote wa serikali ya jimbo hilo
kushirikiana kutoa msaada wa dharura.
Gavana wa jimbo hilo ameitaja hali
kuwa mbaya na ambayo haikutarajiwa.
Watu 176 bado hawajapatikana.
Jamaa na marafiki pamoja na
wafanyakazi wa kujitolea, wanatumia misumeno na mikono mitupu kuondoa vifusi
ili kutafuta wale waliopotea.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment