Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Sekretarieti ya Ajira,Riziki Abraham katika Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma imekamata vyeti feki 1,035 (sawa na asilimia1.6) ya maombi ya
kazi yaliyotumwa kwa miaka minne tangu kuanzishwa kwa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Tangu wakati huo, jumla ya watu 65,000 walijitokeza na
kuomba kazi katika sekretarieti hiyo.
Akizungumza na NIPASHE, Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Sekretarieti ya Ajira, Riziki Abraham, alisema katika
kupokea maombi ya kazi, wamebaini udanganyifu wa hali juu wa vyeti kwa wanaomba
kutoka makazini na wahitimu.
"Tangu miaka minne iliyopita
hadi sasa, Sekretarieti ya Ajira imebaini kuwapo kwa matumizi ya vyeti feki
wakati wa kuomba kazi, barua nyingi zimeonekana kuambatanishwa na nakala
feki," alisema.
Aliongeza: "Ni jambo la
kusikitisha kuona mtu anatumia vyeti ambavyo si vyake kwa lengo la kujipatia
kazi kiudanganyifu au wengine wanajaribu kuongeza vigezo ambavyo hana kwa kazi
anayoomba ambapo husababishwa kutoitwa kwenye usaili,", alisema.
Abraham alisema kuwa ofisi ya
Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa umma inajipanga kutoa elimu kwa
wahitimu na wadau mbalimbali wa elimu katika kuzitatua changamoto hizo.
Aliongeza kuwa sekretarieti hiyo
katika kukabiliana na changamoto hizo wanatarajia kuhama katika mfumo wa
analojia na kwenda dijitali ambapo wahitimu na walio makazini watatuma maombi
kwa njia ya kielektroniki.
No comments:
Post a Comment