John Kerry akutana na Serguei Lavrov
kuhusiana na taharuki kuhusu Ukraine
Waziri wa mashauri ya Nchi za kigeni
wa Marekani John Kerry, amesema kuwa hakuna makubaliano yaliyoafikiwa baina
yake na mwenzake kutoka Urusi Sergei Lavrov, katika mkutano wa
dharurakuhusu mzozo wa Ukraine.
Marekani inasisitiza kuwa hatua ya
urusi kutwaa eneo la Crimea baada ya kura ya maoni sihalali.
Bwana Lavrov ametoa masharti makali
yasiyoegemea upande wowote huku akitaka uhuru wa Ukraine kama taifa utambuliwe.
Waziri wa Urusi amesema kuwa ni
jukumu la Kiev kuandaa katiba mpya ili kuwezesha hilo lifanyike, mbali na
kulinda maisha ya waukraine wachache wanaozungumza kirusi dhidi ya uvamizi
kutoka kwa
waukraine wanaounga mkono kujiunga na
jumuiya ya Ulaya.
Marekani imetaka hatua ya kuongeza
wanajeshi zaidi wa Urusi katika mpaka mashariki ya Ukraine kukomeshwa mara
moja.
Mazungumzo ya Paris siku ya ijumaa
yalifuatwa na mazungumzo ya simu kati ya Rais Vladimir Putin wa Urusi na Rais
Obama wakati aliposimama kwa muda akiwa njiani kuelekea Washington siku ya
Jumamosi, Bwana Kerry alibadilisha
mkondo na kuelekea Paris.
Ukraine inasisitiza kuwa Urusi ina
njama ya kuigawanya Ukraine na kulisambaratisha kama taifa.
Waandishi wanasema kuwa Maafisa wa
Marekani wamegawanyika iwapo mazungumzo hayo yaliyopangwa yametokana na nia
halisi ya Urusi ya kujaribu kupunguza taharuki iliyopo au ni mipango ya
hatua zaidi ya kijeshi.
Pentagon inaamini kuwa maelfu ya
wanajeshi wa Urusi wamekita kambi karibu na mpaka na Ukraine kwa niya ya
kuwatishia viongozi wa Ukraine .
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment