Mahakama ya Misri imewahukumu kifo
wafuasi 528 wa rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Mursi. Wafuasi hao
walikutwa na hatia ya kuanzisha ghasia na kuvamia majengo ya polisi katika mji
wa Kusini mwa Minya.
Wote waliohukumiwa kifo katika kesi
hii ambayo ni kubwa kabisa katika historia ya Misri, wana haki ya kukata rufaa
dhidi ya hukumu hiyo.
Kati ya hao waliohukumiwa 153 wako
kizuizini huku wengine wakiwa bado wanaendelea kutafutwa.
Kesi hiyo ilianza siku ya Jumamosi na
washtakiwa 1200 kutoka chama kilichopigwa marufuku cha Udugu wa Kiislamu
walisimamishwa kizimbani.
Hata hivyo jaji aliyotoa hukumu hiyo
Saeed Youssef aliwaachia huru washtakiwa wengine 17.
Rais wa zamani wa Misri Mohammed
Mursi
Rais wa zamani wa Misri Mohammed
Mursi
Mahakama hiyo aidha iliwagawanya
washtakiwa katika makundi mawili, hukumu ya kundi la pili la washtakiwa 700
inatarajiwa kutolewa hapo kesho.
Kulingana na gazeti linalomilikiwa na
serikali la Al- Ahram watu hao 528 waliohukumiwa kifo walipatikana na hatia ya
mauaji dhidi ya polisi, na kuvamia kituo cha polisi pamoja na kudhibiti silaha
za polisi nchini humo.
Baada ya polisi kuvunja makambi
mawili ya upinzani Agosti 14, mwaka uliopita watu hao pia walishtakiwa kwa
kuvamia watu na mali ya umma kusini mwa mji wa Minya.
Rais wa zamani Misri anakabiliwa na
mashtaka
Morsi, rais wa kwanza wa Misri
aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia alipinduliwa madarakani na jeshi la
nchi hiyo mwezi Julai baada ya maandamano makubwa dhidi ya utawala wake wa
takriban mwaka mmoja.
Maelfu ya wafuasi wake waliuwawa na
wengine kukamatwa wakati wa operesheni kali iliofanywa na serikali dhidi ya
upinzani.
Mkuu wa Majeshi Misri jenerali Abdel
Fattah al-Sisi
Mkuu wa Majeshi Misri jenerali Abdel
Fattah al-Sisi
Mwezi Desemba mwaka jana serikali
inayoungwa mkono na jeshi ililiweka kundi la Udugu wa Kiislamu katika orodha ya
makundi ya kigaidi.
Kwengineko shirika la Kimataifa la
kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limesema takriban watu 1400
waliuwawa katika ghasia za Misri huku wengine zaidi ya 1000 wakitiwa nguvuni.
Rais wa zamani Mohammed Mursi kwa
sasa anakabiliwa na mashtaka katika kesi tatu tofauti, ikiwemo kuchochea mauaji
ya waandamanaji nje ya ikulu ya rais wakati alipokuwa madarakani.
Mursi aliondolewa madarakani baada ya
madai ya kuchukua madaraka kwanguvu na kuyumbisha uchumi dhaifu wa nchi hiyo.
Mwandishi: Amina Abubakar/dpa/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu
Chanzo: DW Swahili
No comments:
Post a Comment