Dar es Salaam. Klabu ya Yanga imeomba
kibali cha kufanya maandamano hadi ikulu kuushinikiza uongozi wa mkoa wa Dar es
Salaam kutoa majibu ya maombi yao heka 11 kwa ajili ya upanuzi wa Uwanja wa
Kaunda.
Katibu wa Yanga, Benno Njovu
aliiambia Mwananchi jana kuwa ameliandikia barua Jeshi la Polisi, Kanda Maalum
ya Dar es Salaam kuomba kibali hicho baada ya juhudi zao za kufuatilia maombi
yao kwenye mamlaka za mkoa kushindikana.
Yanga, klabu kongwe kuliko zote
nchini, ina mpango wa kujenga uwanja wa kisasa utakaojulikana kama Jangwani
Complex, lakini ina ardhi ndogo kwenye maeneo ya Jangwani isiyokidhi mahitaji
ya uwanja huo wa kisasa.
Njovu alisema wameliomba Polisi ili
liwaruhusu kufanya maandamano hayo Machi 17 mwaka huu.
Naye mwanachama anayejulikana kama,
Ibrahim Akilimali, ambaye amekuwa akitambulisha kama katibu wa Baraza la wazee,
alidai jana kuwa maandamano yao yanatokana na kuzungushwa kwa kipindi kirefu
tangu Juni mwaka jana walipoomba ongezeko la eneo hilo licha ya kufikisha ombi
lao kwa kufuata taratbu.
Naye Kamanda wa Polisi wa Dar es
Salaam, Suleiman Kova aliiambia Mwananchi jana kuwa hajaiona barua hiyo kwa
kuwa alikuwa nje ya ofisi eneo ili tujue moja.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment