Mili 25 imepatikana Ziwa Albert baada
ya boti iliyokuwa imebeba wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuzama.
Wakimbizi wa mapigano mashariki mwa
Congo
Wakimbizi hao walikua wakitoroka
kutoka kambi ya wakimbizi ya Kyangwali wilayani Hoima magharibi mwa Uganda,
wakirejea kwao.
Kwa sasa Jeshi la polisi linaendelea
na jitihada za kutafuta miili zaidi. Kamanda wa polisi wa eneo hilo John
Ojukuna amesema watu 43 wameokolewa. Boti iliyozama inadhaniwa kuwa ilikua
imebeba zaidi ya wakimbizi 100.
Wengi wa wakimbizi hao ni wale
waliokimbia mapigano mashariki mwa Congo mwaka jana.
Mwendeshaji wa boti hiyo amekamatwa
na jeshi la polisi na inadaiwa kuwa alikua amelewa. Wakimbizi waliookolewa
wameambia polisi kuwa alikuwa mlevi na alikua akiendesha boti hiyo kwa kasi
sana.
Hii sio mara ya kwanza ajali ya boti
kuua watu katika Ziwa Albert kutokana na kujaza abiria na mizogo kupita
kiasi.Miaka minne iliyopia boto nyingine ilizama na kusababisha vifo vya watu
70.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment