Dar es Salaam. Kampuni ya Microsoft,
inayojishughulisha na utengenezaji wa kompyuta pamoja na programu, imebuni
mbinu mpya ya kukabiliana na wizi wa mitandaoni ambao umezisababishia hasara
benki, kampuni na watu binafsi katika maeneo mengi duniani
Mkakati huo umekuja wakati benki
nyingi nchini zikiathiriwa na wizi huo kupitia mashine za kutolea fedha maarufu
kama ATM pamoja na miamala inayofanyika kupitia mifumo ya mawasiliano ya
kompyuta.
Takwimu zinaonyesha katika kipindi
cha Oktoba 2012 hadi Februari 2013, Tanzania inakadiriwa kuwa Sh700 milioni
ziliibwa katika benki kwa nyakati tofauti.
Kutokana na hali hiyo Gavana wa Benki
Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu aliziagiza taasisi za fedha kuchukua hatua
ili kukabilina na hali hiyo.
Taarifa kwa vyombo vya habari
iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Microsoft, David Finn imeeleza
kuwa wamebuni kompyuta mpya pamoja na programu ambazo zinaziba mianya ya wizi.
Imeweka wazi kuwa uuzaji holela wa programu za kompyuta duniani umekuwa chanzo
cha wezi hao kutumia ujanja katika kufahamu taarifa za siri zilizohifadhiwa
kwenye kompyuta za taasisi na hata watu binafsi zilizounganishwa kwenye
mtandao.
"Kampuni na taasisi na Serikali
zinashauriwa kununua kompyuta mpya kwa mawakala maalumu zitakazowekewa
'software' (programu) zilizo halali," alisema Finn na kuongeza:
"Utafiti uliotolewa mwaka huu na
kampuni ya kimataifa ya teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta ikishirikiana na
Chuo Kikuu cha Singapore unaonyesha, wizi wa kwenye mtandao unagharimu kampuni
zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 315 kwa mwaka sawa na Sh504
trilioni,".
Sehemu ya ripoti hiyo imeeleza kuwa
maeneo mengi ya Afrika yanakua kwa kasi katika matumizi ya mitandao kutokana na
vitendo vya kiharamia na wengi wamejikuta wakipata hasara kwa kuibiwa fedha
zao.
"Wizi wa njia ya mtandao
unahamasishwa na tamaa ya pesa bila jasho kwa kutumia werevu wa teknolojia
kuingilia na kuchukua taarifa muhimu za mtu, kitambulisho, namba za siri au
hata pesa, hivyo Microsoft imedhamiria kudhibiti vitendo hivyo ili kuongeza
usalama wa taarifa za wateja," alisema Finn.
Anasema utafiti umebaini kuwa
kompyuta 203 zilizo nunuliwa katika maduka 11 tofauti, zilibainika kuwa
asilimia 61 ziliathiriwa na programu za kiwizi maarufu kama virusi vinavyoitwa
trojans, worms, viruses, hacktools, rootkits na adware
Chanzo: Mjengwa
No comments:
Post a Comment