Na Miza Kona Maelezo Zanzibar
Mamlaka ya Hali ya HewaTanzania
imewataka vijana nchini kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya
hewa ili kizazi kijacho kiweze kufaidi dunia yenye mazingira bora.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa
vyombo vya habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani ,imewataka
vijana kujihusisha na masuala ya hali ya hewa ili kupata maarifa na uelewa wa
hatua za kuchukua katika kipindi hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
Taarifa hiyo mewataka vijana walioko
mashuleni, vyuoni na wajasiriamali kushiriki katika kuokoa dunia kutoka kwenye
majanga yaletwayo na mabadiliko ya hali ya hewa na chachu kubwa ni kuhakikisha
vijana wanakuwa mstari wa mbele katika kufuatilia taarifa za hali ya hewa
zinazotolewa na Mamlaka hiyo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Siku ya
Hali ya Hewa Duniani ni siku ya kutafakari juhudi zinazochukuliwa na
Wanasayansi Duniani katika kufahamisha Dunia kuchukua tahadhari juu ya
mabadiliko ya hali ya hewa na athari zake.
Mamlaka ya Hali ya Hewa
inawakaribisha wananchi kutembelea vituo vya hali ya hewa nchini ili kuona
shughuli zinazotolewa na Mamlaka hiyo kuanzia kesho
Siku ya hali ya hewa duniani
huadhimishwa kila ifikapo tarehe 23 Machi ya kila mwaka na ujumbe wa mwaka huu
ni Ushirikishwaji wa vijana katika masuala ya hali ya hewa. mwisho
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO.
No comments:
Post a Comment