Taarifa za hivi punde zinasema kuwa
kumetokea mashambulizi makali ya ufyatulianaji risasi mjini Maiduguri Kaskazini
Mashariki mwa Nigeria.
Wakazi wa mji huo wanasema kuwa
walisikia ufyatuaji wa risasi na milipuko kwa karibu saa mbili nyakati za
Asubuhi.
Inaarifiwa tukio hili limejiri
wakati, wa kile kinachoshukiwa kuwa shambulizi dhidi ya kambi ya jeshi
lililofanywa na wapiganaji wa Boko Haram.
Kuna taarifa za mamia ya wapiganaji
kuvamia mji huo asubuhi na mapema na kushambulia kambi mbili rasmi za jeshi ili
kuwaachilia wapiganaji waliokamatwa na kuzuiliwa.
Wakazi walisema kuwa waliona ndege
mbili za jeshi zikipaa katika eneo hilo.
Pia kumekuwa na taarifa ya milipuko
kusikika ndani ya nyumba za wakazi pamoja na katika chuo kikuu cha Maiduguri.
Afisaa mkuu wa haki za binadamu
katika umoja wa Mataifa Navi Pillay -- ambaye yuko nchini humo, alisema kuwa
ukatili unaotendwa na wanajeshi ni sababu ya kundi la Boko Haram kuendeleza
mashambulizi.
Maelfu ya watu wameuawa nchini
Nigeria katika kipindi cha miaka mitano tangu kundi la Boko Haram lilipoanza
vita.
Ghasia hizi zimekithiri katika miezi
michache iliyopita, licha ya juhudi za maafisa wa usalama kuzidhibiti usalama
na kutangazwa kwa hali ya tahadhari katika majimbo matatu.
Chanzo: BBC Swahil
No comments:
Post a Comment