Kampeni ya kimataifa ya kuitenga
Urusi kwa msimamo wake juu ya Crimea inazidi, huku Marekani ikituma meli kwenye
Bahari Nyeusi, nako Crimea bendera za Urusi zikipepea kwenye makao makuu ya
jeshi la majini.
Bendera ya Urusi ikipepea kwenye
makao makuu ya jeshi la majini la Ukraine katika jimbo la Crimea.
Bendera ya Urusi ikipepea kwenye
makao makuu ya jeshi la majini la Ukraine katika jimbo la Crimea.
Rais Vladimir Putin wa Urusi
anakabiliwa na shinikizo kutoka kila upande, ingawa haonekani kutikisika hadi
sasa panapohusika dhamira ya nchi yake kuichukua tena Crimea.
Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe,
amekuwa kiongozi wa hivi karibuni kabisa kupaza sauti yake juu ya hatua hiyo ya
Urusi, wakati akizungumza kwenye bunge la nchi yake hivi leo, ambapo alisema
anashauriana na wenzake wa kundi la mataifa tajiri duniani la G7 juu ya
kukabiliana na Urusi.
"Tunalaani hatua za Urusi ambayo
katika karne ya 18 iliasaini mkataba ambao uliirejesha Crimea kwa Urusi. Na
tunaiona hatua hii ikivunja mamlaka na heshima ya taifa la Ukraine. Japan
haitalichukulia kijuujuu jaribio lolote la kubadilisha hali iliyopo kwa kutumia
nguvu." Alisema Abe.
Tayari Japan ilishatangaza tangu jana
kwamba itasimamisha mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea juu ya uwekezaji na
ulegezaji wa masharti ya viza kati yake na Urusi kama sehemu ya vikwazo vyake.
Kampeni ya kimataifa dhidi ya Urusi
Watu wenye silaha wanaoaminika kuwa
wanajeshi wa Urusi wakilinda makao makuu ya jeshi la majini la Ukraine katika
jimbo la Crimea.
Watu wenye silaha wanaoaminika kuwa
wanajeshi wa Urusi wakilinda makao makuu ya jeshi la majini la Ukraine katika
jimbo la Crimea.
Marekani hivi sasa inaongoza kampeni
za kimataifa kuitenga zaidi Urusi na mkutano wa mataifa ya G7 unaofanyika wiki
ijayo mjini The Hague utajikita kwenye hatua hizo, kwa mujibu wa Ikulu ya
Marekani.
Msimamo kama huo pia umeoneshwa na
Waziri Mkuu wa Australia, Julie Bishop, ambaye ameliambia bunge hivi leo kuwa
hatua ya Urusi kuichukua Crimea haikuwa halali na inapaswa kukabiliwa kwa hatua
kali.
"Serikali ya Australia itaweka
vikwazo kwenye sekta ya fedha na marufuku ya kusafiri kwa wale ambao wamekuwa
mbele katika kitisho cha Urusi dhidi ya mamlaka ya Ukraine. Hatua
zilizochukuliwa na Urusi ni uvunjaji wa wazi wa kanuni za kimataifa
zinazokataza matumizi ya nguvu na kulinda heshima ya mataifa." Alisema
Bishop.
Ukraine yaapa kutoondoa majeshi yake
Crimea
Ujumbe wa Crimea ukiwa kwenye jengo
la bunge la Urusi, Duma.
Ujumbe wa Crimea ukiwa kwenye jengo
la bunge la Urusi, Duma.
Wakati hayo yakiendelea, Waziri wa
Ulinzi wa Ukraine, Ihor Tenyukh, amesema nchi yake haitawaondoa wanajeshi wake
kwenye mkoa wa Crimea, licha ya Rais Putin kutangaza rasmi kuwa Crimea ni
sehemu ya Shirikisho la Urusi.
Kauli hiyo wakati bendera tatu za
Urusi zikionekana kupepea kwenye makao makuu ya jeshi la majini la Ukraine
kwenye bandari ya Sevastopol huko Crimea. Kwa mujibu wa shirika la habari la
Reuters, wanajeshi wanaokisiwa kuwa ni wa Urusi wanalinda makao makuu hayo huku
pia wakiwepo wanamgambo wa "vikosi vya ulinzi", ambavyo vinaundwa na
wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi.
Tayari Waziri Mkuu wa Ukraine, Arseny
Yatsenyuk, amemuamuru naibu wake wa kwanza, Vitaly Yarem, na waziri huyo wa
ulinzi kwenda Crimea kujaribu kutuliza hali na "kuhakikisha kuwa mgogoro
wa Crimea haugeuki kuwa wa kijeshi."
Marekani yatuma meli Bahari Nyeusi
Meli ya kivita ya Marekani, USS
Truxtun, ikiondoka Istanbul, Uturuki, kuelekea kwenye Bahari Nyeusi, kwa ajili
ya kushiriki mafunzo ya kijeshi na Bulgaria na Romania.
Meli ya kivita ya Marekani, USS
Truxtun, ikiondoka Istanbul, Uturuki, kuelekea kwenye Bahari Nyeusi, kwa ajili
ya kushiriki mafunzo ya kijeshi na Bulgaria na Romania.
Wakati huo huo, Marekani imetuma meli
yake ya kivita kwenye mafunzo ya siku moja ya kijeshi kati yake na majeshi ya
majini ya Bulgaria na Romania kwenye Bahari Nyeusi.
Crimea iko kwenye upande wa kaskazini
wa bahari hiyo na Marekani inaiita hatua hii ya leo kuwa ni jambo la kawaida
lililopangwa hata kabla ya kuanza kwa mzozo nchini Ukraine.
Hata hivyo, afisa mahusiano wa Kikosi
cha Jeshi la Marekani barani Ulaya, Shawn Eklund, ameliambia shirika la habari
la Reuters kuwa Marekani inapaswa "kuwaunga mkono washirika wake kwenye
Jumuiya ya Kujihami ya NATO" katika eneo hilo.
Mwandishi: Mohammed Khelef/Reuters/AFP/AP
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman
DW.DE
No comments:
Post a Comment