Wanawake wa Crimea wakiwa Simferopol, Ukraine wakifurahia kujitenga kwao kutoka Ukraine na kuwa sehemu ya Russia
Maafisa katika Jamhuri ya Crimea
iliyojitenga na Ukraine wanasema wapiga kura kwa idadi kubwa wameidhinisha
kujiunga na Russia katika kura ya maoni iliyokuwa na utata ambayo imefanya
viongozi wa magharibi kujiandaa na vikwazo dhidi ya Moscow. Jumatatu bunge la
Crimea liliidhinisha kura ya maoni, kutangaza
uhuru na kuwa rasmi sehemu ya Russia.
Hivi sasa imetangazwa rasmi wa-Crimea
tayari wapo chini ya udhibiti wa Russia na wanaiunga mkono Russia wamefanya
uchaguzi wa kujitenga kutoka Ukraine na kuungana na Russia. Kufuatia kura ya
jumapili ya kujiunga na Russia, bunge la kieneo la Crimea limeomba kuwa sehemu
ya shirikisho la Russia.
Lakini nini kinachofuata baada ya
kura ya maoni, wote viongozi kwenye peninsula ya Black Sea na dunia
waligawanyika katika njia ambazo zinakumbusha mivutano ya enzi ya vita baridi, viko mbali kumalizika.
Wabunge huko Moscow wanaahidi kuweka
kando vikwazo vya kisheria ili kuiruhusu
Crimea kuingia kwenye shirikisho la Russia.
Lakini wasi wasi wa haraka kwa eneo ambalo halina mpaka wa ardhi na
Russia unajumuisha usambazaji wake wa nishati, maji na bidhaa nyingine za
msingi ambazo hivi sasa wanayapata kutoka Ukraine.
Moscow inatetea hatua ya Crimea kama
kuongeza kanuni za kujitambua wenyewe.
Mazungumzo kwa njia ya simu kati ya Rais wa Marekani Barack Obama na
Rais wa Russia Vladimir Putin yanaripotiwa kuleta mafanikio kidogo kuziba
mwanya uliopo.
Waangalizi wa kigeni walioalikwa na
Crimea inayoungwa mkono na serikali ya Russia walitetea kura ya maoni kama
inaendeleza kanuni za kimataifa. Mwangalizi kutoka Ubelgiji, Frank Creyelman
aliwapuuza wakosoaji wakiwemo kutoka serikali mpya huko Kyiv kwamba upigaji kura ulifanyika kwa mtutu wa bunduki.
Chanzo: VOA Swahili
No comments:
Post a Comment