Nyumba ya kifahari ya Jacob Zuma
Chama tawala nchini Afrika ANC kimetoa
kauli yake kuhusu tuhuma za utumizi mbaya wa pesa za Umma dhidi ya Rais Jacob
Zuma.
Katibu mkuu wa chama hicho, Gwede
Mantashe, amesema kuwa afisa yeyote aliyehusishwa na makosa yoyote, lazima
akabiliwe na sheria.
Lakini amepuuzilia mbali wito kuwa
Rais Zuma aondolewe mamlakani au ajiuzulu.
Hapo jana mdhibiti wa mali ya
umma,Thuli Madonsela, alisema kuwa Zuma alitumia sehemu ya pesa za umma
zilizotengewa ukarabati wa nyumba yake kwa mambo yake binafsi.
Thuli Madonsela, aliamuru Rais Zuma
kulipa pesa za ziada alizotumia za umma kukarabati nyumba yake ya kifahari,
akisema kuwa alijinufaisha na pesa za umma kwa njia isiyofaa.
Ukarabati huo, ulijumuisha bwawa la
kuogelea, kliniki binafsi na eneo la helikopta kuweza kutua.
Chama hicho kimesema kuwa ripoti hiyo
imetolewa wakati usiofaa nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu mwezi Mei.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment