Waandishi wa habari nchini Rwanda
Serikali ya Rwanda imekanusha ripoti
iliyochapishwa na shirika la kimataifa la waandishi wasio na mipaka kuihusu.
Ripoti hiyo imeishutumu Rwanda kwa
kunyanyasa waandishi wa habari wa kimataifa pamoja na wale wa nchini humo ambao
kwa miaka mingi hawajaweza kufanya kazi yao katika mazingira huru.
Aidha ripoti hiyo imeshutumu Rwanda
kwa kutotoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu mazingira ya kikazi nchini
humo.
Afisa wa upashaji habari katika bodi
ya kudhibiti habari na uandishi ya Rwanda Gerrard Mbanda amesema ripoti hiyo
inalenga kuipaka matope serikali ya Rwanda.
Ripoti hiyo iliyotolewa Jumatano,
ilisema kuwa serikali hutoa vitisho kwa waandishi wa habari na kutishia uhuru
wa vyombo vya habari kufanya kazi zao.
Kadhalika shirika hilo limemtaka Rais
Paul Kagame kuelewa, kuwa watu wanaweza kutumia njia sawa zinazokubalika
kisheria kukosoa serikali bila ya kukiuka maadili na misingi ya serikali ya
Rwanda.
Shirika hilo liliwataja waandishi
kadhaa ambao lilisema wamenyanyaswa na serikali ya Rwanda.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment