Watu kadhaa wameuwawa na wengine
wengi kujeruhiwa baada ya vurumai kutokea pale walipokuwa wakihudhuria zoezi la
serikali la kuwaajiri watu kazi katika miji kadhaa Nchini Nigeria.
Maelfu ya watu waliokuwa na hamu
kubwa ya kupata ajira, walijitokeza kwa wingi katika zoezi hilo kote Nchini
humo. Walikuwa wamejitokeza katika ofisi za wizara ya uhamiaji.
Walioshuhudia wamesema kuwa karibu
watu saba wamekufa pale umati uliposukumana katika lango kuu la uwanja wa
kitaifa wa michezo mjini Abuja.
Wengine walipoteza maisha yao katika
uwanja wa michezo wa Port Harcourt na uwanja wa shule katika mji wa Minna.
Tatizo la ajira kwa vijana ni kubwa
mno Nchini Nigeria huku zaidi ya robo tatu ya vijana walio na chini ya umri wa
miaka 25 wakiwa bila kazi.
Maelfu ya watu walijitokeza kufanya
mtihani wa ajira - inaarifiwa mkanyagano ulitokea walipojaribu kufika katikati
ya uwanja.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment