Majeshi
ya Somalia na yale ya Umoja wa Afrika
(AU) wamekomboa miji kadhaa kutoka kwa wanamgambo wa Al-shabab katika kile walichokiita juhudi
mpya za kuliondoa kundi hilo kutoka
kwenye ngome zake nchini humo.
Moja
ya maeneo ni katika mji wa Burdhubo ambao
ulikuwa ni ngome kuu ya Alshabab kusini mwa Somalia. Majeshi kutoka Umoja wa
Afrika nchini Somalia yajulikanayo kama AMISOM na jeshi la
taifa la Somalia yalichukua tena
udhibiti wa eneo hilo Jumapili baada ya siku moja ya mapigano.
Kanali
Ali Hamud msemaji wa AMISOM aliimbia VOA kwamba wapiganaji wa Alshabab wanarudi
nyuma mara tu wanapoona majeshi ya AMISOM,
lakini hilo bado linaangaliwa ikiwa badala yake wanajipanga kwa vita vya msituni.
Miji
mingine ambayo jeshi la Somalia na AMISOM wamekomboa tangu Ijumaa ni pamoja na
Weel Dehyn,Wajid,Rabdhure Ted na Hudur. Wako katika mikoa ya Gedo na Bakool
karibu na mpaka wa Ethiopia na kilometa chache kutoka mji mkuu wa Somalia
Mogadishu.
Chanzo:
BBC Swahili
No comments:
Post a Comment