Simbikangwa alikuwa mkuu wa ujasusi wa Rwanda wakati wa mauaji ya Kimbari
Mahakama nchini Ufaransa, imemhukumu
kifungo cha miaka 25 jela jasusi mkuu za zamani wa Rwanda Pascal Simbikangwa
kwa kuhusika na mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Simbikangwa alipatikana na hatia ya
kuhusika na mauaji hayo na kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.
Alikabiliwa na makosa ya kuchochea ,
kupanga na kusaidia katika juhudi za mauaji ya watutsi hasa kwa kuwapa silaha
wapiganaji wa kihutu waliokuwa wanalinda vizuizi vya barabarani na kuwaua
wanaume wa kabila la Tutsi, wanawake na watoto.
Simbikangwa alikanusha madai hayo.
Haijuikani kama mawakili wa
Simbikangwa watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Simbikangwa,mwenye umri wa miaka 54,
anatumia viti vya magurudumu baada ya kuhusika na ajali mwaka 2008 alipokuwa
anaishi katika kisiwa cha Mayotte.
Maelfu ya watutsi na wahutu waliuawa
mwaka 1994
Ni mwanamume wa kwanza kuhukumiwa
nchini Ufaransa kuhusiana na mauaji ya Kimbari Rwanda miaka 20 iliyopita.
Upande wa mashitaka uliitaka mahakama
kumfunga jela maisha Simbikangwa, baada ya kumtaja kuwa mtu mkatili na ambaye
anaweza kufanya mambo mabaya zaidi ya aliyofanya.
Mawakili wake hata hivyo walisema
kuwa kesi hiyo ilishinikizwa zaidi kisiasa na kuwataja mashahidi kama wasioweza
kuaminika na ambao walikuwa na chuki wakati wakitoa ushahidi wao.
Takriban watu 800,000 wengi wao wa
kabila la Tutsi , waliuawa katika kipindi cha siku miamoja.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment