Wiki moja tangu ndege ya Malaysia
iliyokuwa imewabeba abiria 239 kutoweka, juhudi za kimataifa kuisaka ndege hiyo
bado zinaendelea.
Mataifa kumi na mbili sasa yamejiunga
pamoja kuisaidia serikali ya Malaysia na msako huo, juhudi zenyewe zikijikita
zaidi Magharibi mwa rasi ya Malaysia.
Marekani imesema kuwa inatuma
manowari zake za kivita, pamoja na ndege maalum ya uchunguzi katika maeneo ya
Bengal, Bahari ya Andaman na sehemu za Bahari hindi.
Mnamo Ijumaa taarifa ziliibuka kuwa
ndege hiyo ilituma mawasiliano katika kituo cha trafiki ya ndege kwa karibu saa
tano baada ya taarifa ya kupotea kwake kutolewa.
Taarifa zinasema kuwa mawasiliano
hayo yanaweza kusaidia katika kujua iliko ndege hiyo na ndio maana Marekani
ikaamua kutuma meli zake za kivita katika Bahari Hindi.
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment