Rais Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete leo
anatarajiwa kuzindua rasmi shughuli za bunge la kitaifa kuhusu marekebisho ya
katiba mjini Dodoma katika hatua itakayoanzisha rasmi mjadala wa kitaifa kuhusu
marekebisho hayo.
Bunge hilo maalum la katiba limepewa
kati ya siku 70 hadi 90 kujadili rasimu ya katiba na kisha kuifanyia
marekebisho kabla ya kura ya maamuzi.
Kuna ripoti kwamba baadhi ya wajumbe
kutoka upinzani na mashirika ya kiraia yanapanga kuvuruga shughuli hiyo ya
uzinduzi.
Suala la hotuba ya Rais Kikwete
limekuwa sehemu ya mjadala katika Bunge hilo kutokana na baadhi ya wajumbe
kuhoji sababu za Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu kabla ya Rais kuzindua Bunge
kwa mujibu wa kanuni.
Mjadala huo uliwafanya baadhi ya
wajumbe kumzuia Jaji Warioba Jumatatu iliyopita kuwasilisha rasimu hiyo kama
ilivyokuwa imepangwa.
Kikao cha maridhiano kilifanyika siku
hiyohiyo usiku na kufikia mwafaka kwamba Mwenyekiti huyo wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba awasilishe Rasimu ndiposa Rais aweze kuzindua shughuli ya kujadili
rasimu hiyo kabla ya kura ya maoni.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment