Mkuu wa tume ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay
Kamishna wa tume ya Umoja wa Mataifa
ya haki za binadamu ametoa taarifa za kutisha na kuhuzunisha kuhusu ghasia za
hivi karibuni katika Jamuhuri ya Afrika ya kati , baada ya kutembelea taifa
hilo kwa siku tatu .
Navi Pillay amesema watoto katika
taifa hilo wamekuwa wakikatwa katwa vipande na wauaji wamekuwa wakila nyama ya
watu wanao wauwa.
Aliongeza kusema kuwa chuki baina ya
jamii zimefikia kiwango cha kutisha, na kwamba watu wamekua wakiteswa na
kuchomwa .
Hata hivyo amesema kupelekwa huko kwa
vikosi vya Ufaransa na Afrika kumepunguza kiwango kikubwa cha mauaji kwa sasa.
Jamuhuri ya Afrika ya Kati
ilitumbukia katika limbo la ghasia baada ya waasi kuchukua mamlaka mwezi Machi
mwaka jana.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment