Marubani wawili waliokuwa wanaendesha ndege ya Malaysia
Mtambo wa mawasiliano wa ndege ya
Malaysia iliyotoweka wiki moja iliopita, ulizimwa kwa maksudi.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya
waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak.
Taarifa zinazohusiana
Asia
Alisema kuwa ndege hiyo ilibadili
mkondo na kuendelea kuruka kwa saa saba zaidi ya muda uliotakiwa kulingana na
mawasiliano yaliyorushwa kwa Satelite na mtambo wa Radar.
Bwana Razak aliongeza kwamba hatua za
ndege hiyo zinaambatana na matakwa ya mtu binafsi ambaye alikuwa akiielekeza.
Ngege hiyo ilitoweka wiki jana ikiwa
imewabeba abiria 239.
Nusura bwana Razak aseme kuwa ndege
hiyo ilitekwa nyara ingawa alisisitiza kwamba uchunguzi ungali unaendelea
kubaini ilikokwenda ndege hiyo.
Dhana kwamba ndege hiyo ilitekwa
nyara ilipingwa vikali awali lakini sasa inaonekana imerejea kuwa mojawapo ya
sababu za kutoweka kwake.
Mtambo wa mawasiliano wa ndege hiyo
ulizimwa kwa maksudi na huenda marubani walifanya hivyo kwa hiari au kwa kulazimishwa.
Darubini sasa inawalenga watu
waliokuwa wameabiri ndege hiyo na wafanyakazi wa ndege.
Wapelelezi watataka kujua ikiwa
kumekuwa na tukio lolote la matatizo ya kiakili, changamoto za kifamilia na
shinikizo la mawazo kwa yeyote aliyekuwa katika ndege hiyo, hasa marubani.
Ni wiki nne tu zimepita tangu rubani
wa ndege ya Ethiopia kuiteka nyara ndege akitaka kupata hifadhi nchini
Switzerland.
Marubani wa ndege hiyo ya Malaysia
walikuwa na rekodi nzuri tu ya kikazi ingawa polisi bado wamefanya msako
nyumbani kwao.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment