Askari wa kikosi cha Sudan katika jimbo la Darfur
Shirika la haki za binadamu Human
Rights Watch linasema makumi kadhaa ya watu waliuawa katika ghasia
zinazoendelea katika jimbo la Darfur nchini Sudan.
Shirika hilo linasema viongozi wa
kijamii katika vijiji viwili wametoa orodha ya majina ya raia takriban arobaini
waliouawa katika wiki chache zilizopita kwenye makabiliano baina ya vikosi
vinavyounga mkono serikali na vile vya waasi.
Human Rights Watch linasema
wanavijiji wengine makumi kadhaa walishambuliwa, baadhi yao wakipigwa na
makombora ya ndege za kijeshi. Shirika la msalaba mwekundu limesema mmoja wa
wafanyakazi wake aliuawa jana.
Umoja wa Mataifa unasema mwaka huu
pekee zaidi ya watu laki mbili wameyakimbia makazi yao jimboni Darfur.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment