Friday, October 11, 2013

WENGER ATAKA KUSAJILI STRAIKA HISPANIA



KLABU ya Arsenal imejadili uwezekano wa kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa Juventus, Fernando Llorente katika dirisha dogo la usajili Januari mwakani. (HM)
Licha ya timu yake kuanza vizuri mwanzoni mwa msimu, kocha Arsene Wenger bado anataka kusajili mshambuliaji mpya.

Na The Gunners wapo karibu mno kufuatilia maendeleo ya mshambuliaji huyo wa Hispania mjini Turin kuelekea kumsajili mwanzoni mwa mwaka ujao.
Wasaka vipaji wa Arsenal, walimuangalia Llorente kwa mapana marefu misimu ya karibuni na Wenger ni shabiki mkubwa wa mshambuliaji huyo.

Llorente alijiunga na Juventus akitokea Athletic Bilbao mwanzoni mwa msimu, lakini amekuwa akisotea namba kikosi cha kwanza kutokana na uwepo wa Carlos Tevez.
Na Arsenal inataka kutumia nafasi hiyo kwa kumuomba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa mkopo.

Llorente amepoteza nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania na inafahamika lazima apate namba ya kudumu katika klabu ili kujihakikishia nafasi ya kwenda na kikosi cha Vicente Del Bosque kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Na nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza Uwanja wa Emirates itakuwa nafasi ya kukata rufaa kwa Llorente kurejea kikosini Hispania.

Wakati huo huo, Wenger amesema kwamba yuko tayari kusaini Mkataba mpya na Arsenal. 
Chanzo: binzubeiry

No comments: