Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake
Tanzania(UWT), Sofia Simba.
Na Godfrey
Kahango, Mwananchi
Mbeya.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT), Sofia Simba na Mbunge wa Viti
Maalumu, Mkoa waMbeya, Dk Mary Mwanjelwa (CCM), juzi walitumia muda mwingi
jukwaani kumnangaMbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Chadema)
wakimfananisha na `pepo’ aliyekwenda bungeni kwa ajili ya kufanya vurugu.
Viongozi
hao walisema kuwa wananchi wa jiji hilo wamepeleka ‘pepo’ bungeni ndio maana
mbunge huyo amekuwa kinara wa vurugu
ndani ya Bunge, hivyo wananchi wa Mbeya Mjini wamempeleka mtu anayehitaji
kuombewa.
Walitoa
kauli hiyo juzi wakati wakihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo
la wazi la Kata ya Manga
Mjini
Mbeya.
Simba,
ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, alisema hali hiyo
ya ‘mapepo’ mara kadhaa imekuwa
ikimsababishia mbunge huyo kujiingiza kwenye vitendo vya vurugu,
likiwemo tukio la hivi karibuni kupigana bungeni badala ya kuibua hoja za
maendeleo. Juhudi za gazeti hili za kumtafuta Sugu zilikwama jana baada ya
kuelezwa na watu wake wa karibu kuwa alikuwa safarini China.
Simba
alisema tukio la mbunge huyo kupigana na askari wa bunge ndani ya ukumbi,
lilitokea kwa kuwa hakukuwa na mtu wa kuombea ‘mapepo’ siku hiyo baada ya
kumkumba ghafla mbunge huyo.
“Siku
ile tukio linatokea bahati mbaya sana
Mchungaji Lwakakatare
(Mbunge wa Viti Maalumu Getrud
Lwakatare) hakuwemo ukumbini maana angeweza kuyaombea na hivyo naomba wananchi
wa Mbeya msituletee ‘mapepo,” alisema.
No comments:
Post a Comment